contact

husen

Wednesday, May 23, 2012

MISS CHANG'OMBE KUFAHAMIKA MWEZI MAY

Mashindano ya kuwania taji la Redds Miss Tanzania
 2012 yanazidi kupamba moto kwa ngazi za vitongoji 
nchini kote huku vitongoji kadhaa vikiwa
tayari vimesha fanya mashindano yake na
 vingine vikiendelea na maandalizi. 
Wakati wiki hii Mashindano hayo yakitraji
 kufanyika 
katika Vitongoji vya Kurasini Jijini Dar es Salaam
 tayari Wanyange wanaowania taji la Redds
 Miss Cha'gombe 2012  nao wapo katika mazoezi
 tayari kwa fainali zao zitakazo fanyika
 mapema mwezi ujao.
Pichani ni warembo wa Chan'gombe wakiwa
 katika picha ya pamoja iliyopigwa muda mfupi 
baada ya kumaliza mazoezi yao Mei 22,2012 
 katika ukumbi wa TCC Chan'gombe jijini Dar es Salaam.
Warembo hao 11 wanataraji kupanda jukwaani
 mapema mwezi ujao kuwania taji hilo na 
kuwania tiketi ya kushiriki Miss Temeke 2012. 

No comments:

Post a Comment