Joh
Makini amerudi kwa kishindo na ngoma yake
iitwayo Manuva na iliyotengenezwa na
mtayarishaji
mkongwe Ambrose aka Dunga.
Tumepiga
story na Joh Makini aka Mwamba
wa kaskazini kuhusu masuala mawili
matatu kama
ifuatavyo.
Kuhusu
wapi aliporekodi Manuva, anapoishi na
anachofanya producer Dunga
Manuva
tumeifanyia pale kwa Dunga nyumbani ana
microphone yake, amegonga beat
nyumbani ana
monitors (speaker) kwahiyo tukafanya pale,
halafu tukaenda kufanya
final mixing na
mastering kwenye studio za B’Hits kwa
Hermy B. Dunga anaishi
Mikocheni. Anafanya
production na kazi zake binafsi.
Kuhusu
wasanii wa Hip hop kutopiga show
za hela kama wanazofanya wasanii wa kuimba
kama Diamond
Mimi
nafikiri hiyo ni kwa wadau tu ambao industry
wanaiona hivyo lakini kwa upande
mwingine
nafikiri watu wa hip hop pia wengi wako smart
sana kibiashara na watu
wenye misimamo
mara nyingi, sasa hiyo kwenye industry inakuwa
kama shida
fulani hivi.
Kuhusu
mipango ya Weusi
Weusi
tuna hii albam yetu ya pamoja ya Weusi,
baada ya hapo kila mtu anaenda solo
sasa, lakini
kampuni inabaki pale pale kufanya biashara za
Weusi kama kuuza
nguo za Weusi na cds.
Kuhusu
kama biashara hizo zinawalipa
Yeah
inatulipa, faida ipo kwasababu tunanunua bidhaa, tunaitengeneza,tunauza kwa
kiasi fulani cha
hela ambacho kina faida pale juu yake, na sio
mbaya
inatusaidia kidogo mafuta ya gari na
vitu vidogo vidogo kuendesha maisha. Sisi
t-shirt zetu tunaziuza kwenye maduka ya watu
tu yaani kama Born 2 Shine, kwa CP
jembe pale
Mwenge kwahiyo tuna washkaji zetu wenye
maduka, tukitoa mzigo
tunawapelekea kwenye
maduka yao kwasababu nao wanapenda
kusupport hip hop,
kwahiyo tunafanya nao
biashara kwa style hiyo.
Kuhusu
kitu asichokipenda kwenye muziki wa sasa
Upigwaji wa nyimbo kwenye radio
stations, nyimbo
zinakuwa hazidumu. Wimbo unatolewa, unapigwa
wiki,unapigwa
wiki inayofuata wiki nyingine
zinakuwa hazipigwi tena. Yaani hakuna upigwaji
ambao unaweza kuufanya wimbo uishi. Kuna
ngoma kama za Hip hop usipozipiga mara
nyingi
watu hawawezi kuelewa sababu utakuta kuna
metaphors,mle ndani kuna
mashairi magumu,
mtu anatakiwa ayasikike mara mbili, mara tatu
ili aweze
kuyatafakari na kuyaelewa. Nadhani
tunahiji airtime nzuri kwaajili ya watu
kuelewa
hiki tunachokuwa tunakiongea kwenye mistari yetu
tofauti na wasanii
wengine wa kuimba sababu wao
muziki wao unategemea tu melody sio katika
uandishi.
Kwahiyo watu wakishapenda melody basi wimbo
unahit lakini wimbo wa
hip hop kama watu
hawajaelewa maishairi inakuwa kidogo kazi.
No comments:
Post a Comment