Msanii
wa filamu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kituo cha
Mafunzo ya Filamu
cha Tanzania Film Training Centre (TFTC)
Emmanuel Myamba maarufu
kama Pastor Myamba akiwasilisha
mada kwenye Jukwaa la Sanaa wiki
hii. Kushoto kwake ni Katibu
wa Shirikisho la Filamu nchini Wilson
Makubi
Na Mwandishi Wetu
Wadau
wa Sanaa wamehoji uhalali wa wasanii wa filamu kutumia
kiingereza
kwenye majina ya filamu zao huku wakishangazwa na
kazi hizo kubeba
maudhui ya kizungu zaidi.
Wakizungumza
wiki hii kwa nyakati tofauti
kwenye programu
ya Jukwaa la Sanaa, wadau
hao walishangazwa
kitendo cha filamu
hizo kutumia majina ya kizungu
wakati hapa kwetu kuna filamu
nyingi kutoka nje zinazotumia lugha
za
kihindi, kichina, kifaransa
na zinafanya vizuri.
“Hoja
kwamba, wanatumia majina ya kiingereza ili kuteka soko la
kimataifa ni
ya kitoto, mbona hapa kwetu kuna filamu nyingi
za kihindi na kichina
zinanunuliwa kwa wingi? Hapa kuna udhaifu
katika kutengeneza filamu
zenye ubora tujikite huko”alisema
Mzee Nkwama Bhallanga.
Kwa
mujibu wa wadau wengi waliozungumza,
filamu ni taaluma
inayozungumza
kwa kutumia picha na
vitendo zaidi hivyo haihitaji
mtazamaji kufahamu
lugha iliyotumiwa
ili afahamu maudhui na ujumbe
unaowasilishwa na kazi
husika ya filamu.
“Maneno
kwenye filamu si muhimu
sana, kinachozungumza
ni matendo
na picha
zaidi, ndiyo maana kuna watu wanaangalia
picha za Kikorea na
wanaburudika na kuelewa kinachoendelea”
alisema Godfrey Lebejo
ambaye ni
Murugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo
na habari, BASATA.
Aliongeza
kuwa, kinachoitesa tasnia ya filamu kwa
sasa ni kukosekana kwa weledi
na uhalisia wa
tamaduni zetu kunakosababishwa na wimbi kubwa
la watu
kujiingiza kwenye filamu ili kufanikisha
mambo yao yaliyo nje ya maadili
na utamaduni wetu.
“Inawezekana
vipi utengeneze filamu ambayo baba,
mama na watoto hawawezi kukaa
pamoja kuitazama?
Tufike mahali tuseme mambo haya ya kipuuzi
basi kwenye
filamu zetu” alionya Lebejo.
Awali akiwasilisha mada kuhusu Filamu, wasanii
na haja ya kujiendeleza kielimu, Msanii
wa
filamu Emmanuel Myamba maarufu kam
Pastor Myamba alisema kuwa,
tasnia ya
filamu inakosa weledi hivyo
kuhitaji mabadiliko.
“Ni
wazi ukiangalia filamu zetu zinakosa weledi katika
uandishi wa miswada,
uongozaji, uhariri na hata
uumbaji wa wahusika. Lazima tukubali udhaifu
huu
turekebishe” alisema Myamba ambaye kwa sasa
amefungua kituo cha
mafunzo ya filamu kiitwacho
Tanzania Film Training Centre (TFTC)
kilichoko Ubungo.
SOURCE DJ CHOKA
No comments:
Post a Comment