contact

husen

Wednesday, July 4, 2012

MWANACHUO WA CHUO CHA UALIMU ST.AGREY MBEYA AUAWA BAADA YA KUTUHUMIWA KUIBA PIKIPIKI


Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo PRAY GOD MGONJA
Mwananchuo wa chuo cha ualimu cha ST Aggrey 
kilichopo uyole jijini mbeya
 anasadikiwa kufariki dunia baada ya kupigwa na 
wananchi wenye hasira kali 
katika maeneo ya Isanga kwa tuhuma zakuiba
 pikipiki zakusafirishia abiria
 maarufu kama bodaboda. 

Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo 
PRAY GOD MGONJA amemtaja mtuhumiwa
 huyo kuwa ni VEDASTO PIUS anayekadiriwa
 kuwa na umri kati 25 mpaka 30 . 

Mgonja amesema tukio hilo limetokea mnamo
 july 2 mwaka huu majira ya saa 8
 za mchana katika daraja lilopo karibu na 
hotel ya Rift Valley barabara yakuelekea
 isanga jijini mbeya. 

Amesema mtuhumiwa 
amekumbwa na mkasa huo 
baada yakupewa taarifa za
 kuibiwa kwa pikipiki yenye No T 438BZU aina
 T-BETTER yenye alama ya
 chama cha Demokrasia na maendeleo mali ya 
JOSEPH KAPASI(23)mkazi 
wa Ilomba jijini hapa

 
Kwaupande wake mmiliki wa pikipiki hiyo 
JOSEPH KAPASI amesema aliombwa
 kumfundisha mtuhumiwa huyo na baadae 
alipoanza kuendesha vizuri alitokomea
 nayo na marabaada ya hapo alipatikana eneo la
 isanga akielekea barabara ya
 chunya ili aibe na ndipo akakamatwa na 
wanainchi wenye hasira kali nakuanza
 kumpa kichapo ambacho kimemfanya azirai


source thechoice

No comments:

Post a Comment