contact

husen

Friday, August 17, 2012

TBC YAOMBA RADHI

Mkurugenzi wa TBS Bw Clement Mshana

Shirika la utangazaji Tanzania, TBC, leo limewaomba
radhi waislam nchini kwa kutoa takwimu zisizo sahihi
 za waislam na wakristu.
Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Clement Mshana
 amefafanua kupitia kipindi cha Jambo Tanzania leo
 asubuhi kwa kukiri kuwa mmoja wa watangazaji wa
TBC1 alitaja takwimu za wakristu kuwa ni asilimia 52%
na waislam asilimia 32% zilizopatikana kutoka
 mtandao wa Wikipedia.
                          TBC imeomba radhi kwa kuwapotosha watanzania
kwakuwa takwimu hizo sio sahihi.
Mshana alikiri kuwa TBC ilifanya kosa kuunukuu mtandao
 wa Wikipedia na kudai kuwa chombo chenye
mamlaka na cha kuaminika ni Wakala wa Takwimu
nchini na sio wikipedia.
Mkurugenzi huyo amesema tarehe 15, May, 2012 shirika
hilo liliandika barua ya kuomba radhi kwa jumuiya ya
waislamu nchini na kumpa onyo mtangazaji aliyetaja
 takwimu hizo.
Ametaka waislam kusahau yaliyopita na kuutumia
mwezi huu wa Ramadhan kusamehe huku akiwataka
wananchi kujitokeza zaidi kwenye zoezi la sensa
litakalosaidia kupatikana kwa takwimu sahihi.

No comments:

Post a Comment