Roy Hodgson ameanza kuiongoza timu
ya taifa ya England vyema
kama meneja, kwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya
Norway,
katika uwanja wa mjini Oslo wa Ullevaal.Bao la Ashley Young
limempa
nguvu meneja Hodgson katika mechi yake ya kwanza
kama meneja wa EnglandKabla ya
mechi hiyo, England ilikuwa
imeshindwa kuishinda Norway katika kipindi cha
miaka
32 iliyopita.Ashley Young ndiye aliyefunga bao hilo la pekee
katika mechi
hiyo, katika dakika za mwanzomwanzo za mechi
hiyo ya kirafiki. Hodgson alipata
nafasi nzuri ya kuwatizama
wachezaji wa England ambao ataweza kuwashirikisha
zaidi
katika juhudi zake za kuisuka vyema timu yake itakayoshiriki
katika
mashindano ya Ulaya ya Euro 2012, baada ya kuchukua
kazi hiyo kutoka kwa Fabio
Capello.Timu ya England
ilionyesha nidhamu ya hali ya juu na anayoitazamia
Hodgson, lakini wengi bila shaka wanafahamu timu
ambayo England itakutana nayo,
Ufaransa, tarehe 11
mwezi Juni katika mji wa Donetsk, haitacheza sawa na
timu
waliyopambana nayo mjini Oslo.Lakini yalikuwa ni
mazoezi ya kuridhisha kwa
Hodgson, ambaye sasa ataweza
kukinoa kikosi chake vyema zaidi katika mechi
nyingine
ya kirafiki katika uwanja wa nyumbani wa Wembley,
Jumamosi ya tarehe 2
Juni, wakati England
itakapoikaribisha timu ya taifa ya Ubelgiji.
Chanzo BBc Swahili
No comments:
Post a Comment