Rais Obama ameongoza katika sifa na rambi-rambi zilizotolewa
baada ya kifo cha
Neil Armstrong, mwana anga wa kwanza kutua
kwenye mwezi, ambaye amefariki akiwa
na umri wa miaka 82
kutokana na matatizo aliyopata baada ya upasuaji
aliofanyiwa
kwenye moyo.
Rais Obama alimuelezea Neil Armstrong kwamba ni mmoja
kati ya mashujaa
wakubwa wa Marekani, siyo wakati wake tu,
lakini katika historia ya nchi hiyo
piya.
Mwenzake Armstrong katika safari ya kihistoria ya kwenda
mwezini mwaka wa
1969 alikuwa Buzz Aldrin, ambaye alisema
Armstrong alikuwa rubani na kamanda
mahiri.
Familia ya Neil Armstrong imetoa wito kwa Wamarekani kuonesha
heshima zao kwa
kufuata mfano wake wa kutumika
, kufanikiwa na bila ya majivuno.
Taarifa ya familia iliwaambia wale washabiki wake:
"ukitembea nje usiku
ukaona mwezi unakuchekea,
mfikirie Neil na umkonyeze."
picha na stori kwa hisani ya bbc
picha na stori kwa hisani ya bbc
No comments:
Post a Comment