wajumbe wa kamati ya
utendaji ya klabu ya Yanga
wakizuia kujiuzulu kwa mwenzao Mohammed Bhinda
(pichan),
badala yake wajumbe hao walimtaka mwenyekiti wa
klabu hiyo Lloyd Nchunga
kujiuzulu.
Maamuzi hayo
yalifikiwa juzi katika kikao cha kamati ya
utendaji ya Yanga kilichoketi kwa
ajili ya kujadili
mustakabali mzima wa hali tete inayoendelea ndani
ya klabu
hiyo, pamoja na barua ya masharti waliyopewa
na aliyekuwa mfadhili wa klabu
hiyo Yusuf Manji.
Habari
zilizopatikana toka ndani ya kikao hicho zinaeleza kwamba,
baada ya Bhinda
kuwasilisha barua yake ya kujiuzulu,
wajumbe hao wakiongozwa na Salum Rupia
walizuia
zoezi hilo kwa madai ya kwamba kiongozi huyo
ni muhimili mkubwa ndani
ya uongozi huo.
Imeelezwa kuwa,
pamoja na kugoma huko, wajumbe
hao walidai kuwa ni heri Nchunga ajiuzulu kwani
ndiye
anayelalamikiwa zaidi na wanachama wa klabu
hiyo lakini si Nchunga hivyo
kumshauri aachie ngazi.
Mmoja ya
wajumbe hao alieleza kwamba baada ya
kumsauri Nchunga kuachia ngazi
aliwaomba wampe
siku mbili au tatu afikirie zaidi ushauri huo kabla ya
kutolea uamuzi.
“NI kweli
tulizuia barua ya kujiuzulu kwa Bhinda kwani
bila yeye hakuna lolote katika
uongozi wa Yanga na
tulimshauri Nchunga ajiuzulu kwani matatizo
yote hayo na
kelele kutoka kwa wanachama
vinamlenga yeye,”alisema mjumbe mmoja.
“Kama
tusipomshauri afanye hivyo itakuwa ngumu
kufanuikisha mambo mengi ambayo
yanaikabili timu yetu
yanayohitajika kufanyika haraka iwezekanavyo na kwa
hali
yake ya kuendelea kuwepo ndani ya Yanga kutafanya
mambo yaendee kuwa magumu
zaidi,”aliongeza .
Kikao hicho
kilihudhuriwa na wajumbe wachache baada ya
wengi wao kutangaza kubwaga manyanga
kutokana na
kuchoshwa na hali ya sintofahamu inayoendelea ndani ya
klabu hiyo,
ambapo tayari Makamu Mwenyekiti Davis Mosha
, pamoja na wajumbe Seif
Ahmed, Ali Mayay,
Bhinda na Mzee Yusuf walitangaza kung’atuka
Kwa sasa Yanga
imebaki na wajumbe wanne, wakimo
Sarah Ramadhani,Tito Osoro, Charles
Mgondo, na Salum Rupia.
Hata hivyo,
Nchunga ambaye jumapili iliyopita
alivuliwa madaraka hayo na wanachama zaidi
ya
700 waliokutana makao makuu ya klabu hiyo
iliyopo mitaa ya Jangwani na Twiga,
hakupatikana
kuzungumzia suala hilo baada ya simu yake
kuita bila kupokelewa.
Hivi karibuni,
uongozi wa Yanga ulijikuta katika
msigano na wanachama wa Yanga wakiongozwa
na
baraza la wazeee na baadhi ya vijana wakitaka
ujitoea madarakani kutokana na
kushindwa kuiletea
mafanikio timu hiyo ambayo ilijikuta ikiutema
ubingwa wake
wa ligi kuu bara ulionyakuliwa na
mahasimu wao Simba na yenyewe kuishia nafasi
ya tatu.
Aidha, uongozi huo
unadaiwa kushindwa kuwalipa
wachezaji pamoja na viongozi wa benchi la ufundi
hatua ambayo imepelekea benchi la ufundi kuachia ngazi,
huku klabu hiyo ikiwa mbioni
kutaifishwa na
mahakama kuu baadhi ya
mali zake kutokana na deni la milioni
106.
Tayari Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF) lilikemea
mapinduzi yaliyofanywa na wanachama wa Yanga kwa
madai ya kukiuka kanuni, huku wakidai kutotambua
mapinduzi hayo na kuwataka
wanachama hao kutumia busaya katika
kutatua suala hilo.
Hata hivyo, wazee hao
wametishia kuifuta Yanga
TFF na kuihamishia Visiwania Zanzibar, pia kuwasilisha
ombi maalum kwa taasisi ya kuzuia na kupambana
na rushwa (TAKUKURU) ili
imchunguze Nchunga kwa
madai kuwa huenda kuna ubadhirifu anaoufanya
ndiyo maana
hataki kung’oka Yanga.
|
No comments:
Post a Comment