Mitt Romney ameteuliwa rasmi kama mgombea urais wa chama
cha
Republican katika kongamano la chama hicho huko Tampa, Florida.
Wajumbe
kutoka majimbo yote ya Marekani walikusanyika
kuthibitisha kumuunga mkono gavana
huyo wa zamani
wa jimbo la Massachusetts.
Atakabiliana na Barack Obama katika
uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba.
Kura ya maoni ya hivi karibuni inaonyesha
wagombea hao
wawili Bwana Romney na rais Obama wakipimana nguvu kwa
karibu.
Bwana Romney, 65, alihitaji kupata japo kura za wajumbe
1,144 ili
aweze kuteuliwa kama mgombea wa chama chake,
na kura za kutoka jimbo la New
Jersey zilimuweka "katika nafasi nzuri".
Dakika chache baadaye, mjumbe wa
bunge la congress wa
Wisconsin Paul Ryan akateuliwa rasmi kuwa mgombea wa
kiti
cha makamu wa rais wa chama cha Republican.
Fursa ya Ann Romney
Bwana
Romney aliteuliwa na wajumbe ambao walikuwa
wakitangaza kura za majimbo yao kwa
sauti hadharani.
Kwa ujumla, Bwana Romney alipata kura 2,061, Spika wa
bunge
la waakilishi John Boehner alitangaza katika kongamano hilo.
Bwana Romney
hakuwepo kwenye kongamano hilo,
lakini alifuatilia kuhesabiwa kwa kura akiwa
katika
hoteli ya karibu yeye na mkewe.
Uteuzi wake huko Tampa unathibitisha
rasmi kuidhinishwa
na chama chake kufanya kampeni.
Waliozungumza kwenye
kongamano hilo walimshambulia rais Obama.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya
chama cha
Republican Reince Priebus alisema rais hajawahi
"kusimamia kampuni.
Hajawahi hata kusimamia karakana."
Wakati huo huo, Bwana Boehner amesema:
"utendaji kazi wa rais Obama si wa kiwango cha kusifiwa."
Siku ya Jumanne
jioni, Ann Romney pia pamoja na Gavana
wa jimbo la Carolina Kusini Nikki Haley
na
Gavana wa jimbo la New Jersey Chris Christie walizungumza
No comments:
Post a Comment