Michuano ya Ligi ya
Taifa inayoshirikisha mabingwa
wa mikoa inaanza Mei 27 mwaka huu katika vituo
vitatu tofauti huku Ashanti United ya Ilala na
Polisi ya Mara zikifungua dimba
katika Kituo cha Musoma.
Ligi hiyo ambayo
inatarajia kumalizika
Juni 12 na 13 mwaka huu itashuhudia mechi
mbili kwa siku
katika kila kituo, huku ya kwanza
ikichezwa saa 8 mchana na kufuatiwa nay a
pili 10 jioni.
Mechi za ufunguzi
Kituo cha Musoma ambapo
mechi zake zitachezwa Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume
mjini Musoma
ni Flamingo ya Arusha dhidi ya Forest ya
Kilimanjaro (saa 8
mchana) wakati saa
10 jioni ni Ashanti United na Polisi.
Kituo cha Kigoma siku
ya ufunguzi
kutakuwa na mechi moja tu itakayoanza saa 10
kamili jioni kwenye
Uwanja wa Lake Tanganyika
kati ya Mwadui ya Shinyanga na JKT
Kanembwa ya
Kigoma. Siku inayofuata ni CDA
(Dodoma) vs Majimaji ya Tabora (saa 8 mchana)
na
Bandari ya Kagera vs Pamba ya Mwanza (saa 10 kamili jioni).
Tenende ya Mbeya na
Kurugenzi ya Iringa
ndizo zitakazoanza saa 8 mchana kwenye
Kituo cha Mtwara na
kufuatia na mechi kati ya
Mpanda Stars ya Rukwa na Ndani ya Mtwara
kuanzia saa
10 kamili jioni. Mechi hizo zitachezwa
katika Uwanja wa Umoja.
|
No comments:
Post a Comment