contact

husen

Friday, May 25, 2012

MWANAMKE ABEBA MIMBA KWA MIAKA 4


Na Ashura Mohamed 

Mwanamke mmoja a julikanae  kwa jina la Chausiku Selemani(48) mkazi
 wa maji ya chai mkoani arusha yuko katika hali ya sintofahamu
 baada ya  kubeba mimba ya miaka minne ambayo amepewa na mtoto
 wa 17  na hadi sasa  hajui siku ya kujifungua , hali ambayo
 imemfanya kuwaomba watu wenye mapenzi mema kujitokeza
 kumsaidia ili aweze kufanyiwa upasuaji.

Chausiku ameyasema hayo nyumbani kwake alipokuwa akiongea 
 kuhusiana na hali aliyonayo ambayo imemfanya asijue la
 kufanya huku akiwa anakabiliwa na hali ngumu ya maisha.
Amesema kuwa  katika maisha yake uzazi wake umekuwa wa
 shida kwa kuwa kila anapozaa mtoto ni lazima tumboni kibakie
 kiumbe cha miezi miwili hali inayompelekea kuzaa kila mwaka
 hadi kufanya kufikia  watoto 16 ambapo kati ya hao watatu
 walishafariki dunia  .“Mimi mara ya mwisho kujifungua ilikuwa
 mwaka 2008 ambapo mara tu baada ya kujifungua nilimwambia
 daktari aniangalie kuna kitu kimebaki tumboni ,alivyoangalia 
aliniambia ni uvimbe upo hivyo nahitajika laki tatu na nusu ili
 nifanyiwe upasuaji lakini kutokana na hali niliyokuwa nayo
 sikupata fedha hizo hali
 iliyopeleka kiumbe hicho kukua hadi leo hii ni mtoto  
namsikia kabisa akichezal akini kila nikipimwa haonekani”
alisema chausiku
Aliongeza kuwa ilimlazimu  aenda katika hospitali ya rufaa ya
 mkoa wa Kilimanjaro (KCMC)   na ndipo  madaktari wa kafanikiwa
 kumkata mirija ya uzazi ili kuthibiti hali hiyo lakini cha
 kushangaza uvimbe huo uliendelaea kukua hadi leo hii  
 ambapo  ameeleza kuwa kukatwa kwa mirija hiyo huenda ndio
 chanzo cha ujauzito huo ku kaa tumboni kwa miaka minne.
Kupitia hali hii mama huyo amewaomba watu wenye mapenzi
 mema wa msaidie kwa lolotelile ikiwa ni pamoja na maombi
 ili kumwezesha  kwenda kufanyiwa upasuaji ili aweze kutolewa
 kiumbe hicho ambapo kimemfanya hata kushindwa  kuwahudumia
 watoto waliopo kwani ni wadogo na kipato cha mume wake hakitoshelezi.

“Hapa kwangu hali ni mbaya sana kwani hata watoto hawana
 hata sehemu ya kulala na wengine wanasoma shule
 hawana hata sare za shule hivyo naombeni hata mkinisaidia
 kwa maombi naamini mungu atanisaidia “aliongeza
Wasamaria wema wanaweza kutuma mchango wao wa m-pesa
 kupitia nambari ya simu ya mume wake ambaye ni
 Elidaima Kimoso 0764-65 02 88.

No comments:

Post a Comment