Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetuma salamu za rambi mbali kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Magesa Muhongo kutokana na vifo vya wananchi watatu wa Mkoa huo vilivyotokea kufuatia mripuko wa bomu uliotokea juzi katika viwanja vya Soweto Jijini Arusha.
Watu
wasiopungua 70 waliripotiwa kujeruhiwa wakati wa mripuko huo kwenye
mkutano wa hadhara wa kampeni za uchaguzi katika Kata ya Soweto wa Chama
cha Demokrasia ya Maendeleo { Chadema }.
Katika
Taarifa ya rambi rambi ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliyotumwa
kwa Mkuu huyo wa Mkoa wa Arusha na kutiwa saini na Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alielezea kupokea kwa masikitiko
na huzuni taarifa ya shambulio la kigaidi la bomu lililotokea tarehe 15
Juni mwaka 2013.
Balozi
Seif alisema Taifa kwa mara nyengine tena limekumbwa na msiba wa njama
za kigaidi zilizoua na kujeruhi rMkuu wa Koa wa Arusha aia wema wasio na
hatia sambamba na tukio jengine linalofanana na hilo lililogharimu roho
za wananchi wengine wakati wakiwa katika ibada Kanisani.
Balozi
Seif alisema kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Wananchi
na yeye binafsi anatuma salamu hizo za rambi rambi kutokana na maafa
hayo na kuwaombea marehemu malazi pema na majeruhi wapone haraka ili
waungane na wenzao katika ujenzi wa Taifa.
Halkadhalika
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar inaiunga mkono Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
katika jitihada zake za kupambana na ugaidi wa aina yoyote hapa Nchini.
Alieleza
kwamba SMZ na Wananchi wa Zanzibar wako pamoja na wenzao katika kipindi
hiki kigumu cha huzuni na maombolezo na kuwaomba wafiwa wawe na moyo wa
ustahamilivu, uvumilivu na subra katika kipindi hichi.
Serikali
ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kutenga shilingi Milioni
Mia Moja { 100,000,000/-} kama zawadi kwa kwa mtu ye yote atakayetoa
Taarifa zitakazofanikisha kunaswa kwa mhalifu au watu wenye mtandao wa
ulipuaji wa mabomu hapa Nchini.
No comments:
Post a Comment