Taarifa zilizotufikia katika chumba cha habari zinaeleza kuwa wanafunzi wanne wa chuo kikuu cha Dar es salaam maarufu kwa jina la Chuo cha Mlimani wamevamiwa na majambazi usiku wa kuamkia leo maeneo ya Yombo chuoni hapo.
Wanafunzi
hao wanaosemekana kuwa ni wa mwaka wa nne na wa mwisho wa masomo
walikuwa wanajisomea na kuandaa “Disertation” zao na kujikuta wakivamiwa
na watu wanne na kuamuriwa watoe komputa zao na pochi za fedha. Kwa
mujibu wa chanzo cha habari hii kutoka chuoni hapo, wanafunzi hao
walikubali kuwapa komputa hizo na pochi za fedha, na majambazi kuanza
safari yao.
Baadaye
wanafunzi hao wakawaomba wapate hata nakala (Soft Copy) ya vitu vyao,
na ndipo mmoja wao akaamua kuwafuata na kukumbana na risasi tumboni. Mwanafunzi huyo baada ya kupigwa risasi alianguka chini na kugaagaa chini huku akikosa msaada wa kupelekwa Hospitalini.
Chanzo
kimeendelea kusema kuwa wanafunzi wa Chuo hicho waliwasiliana na
uongozi ili kupata gari ili wamkimbize mwenzao Hospitalini, lakini
ilipita takribani nusu saa hakuna majibu na ndipo walipoamua kujikusanya
na kuamua kuwafuata viongozi. Kwa sasa mwanafunzi huyo amekimbizwa Hospitalini kupata matibabu zaidi na mpaka sasa hakuna taarifa yoyote iliyotoka, ingawa FULLSHANGWE inajitahidi kufuatilia suala hilo ili kupta taarifa zaidi na picha za tukio hilo.
Tukio
hilo limelaaniwa vikali na UMMA wa chuo kikuu cha Dar es salaam na
kuitaka serikali kufuatiliwa na kudhibiti vitendo hivyo vya kikatili
chuoni hapo. Endelea kufuatilia katika mtandao huu amboa umefunga safari ya kuelekea Chuo kikuu cha Mlimani kuangalia nini kinaendelea.
Mbali
na tukio hilo, pia kumekuwepo na wizi wa hadharani katika shule za Chuo
hicho ambapo hivi karibuni wanafunzi wamekuwa wakiporwa komputa zao
mchana kweupe maeneo ya Mikocheni wakitoke shule kuu ya uandishi wa
Habari na Mawasilinao ya Umma (SJMC).
Suala hizi limepoteza amani kwa wanafunzi na kuwafanya washindwe kusoma kwa amani.
No comments:
Post a Comment