Benki ya
maendeleo ya Afrika (AFDB)inatarajia kutumia
kiasi cha Shilingi bilioni 12
katika mkutano wake unaoanza
Jumatatu jijini Arusha na kufunguliwa na Raisi
Jakaya Kikwete huku kiasi cha fedha hizo zikitumika
kukarabati Kumbi
mbalimbali za jengo la Kimaitaifa
la ukumbi wa AICC kwa kuwa baadhi ya kumbi za
jengo hilo zinaonekana kupitwa na wakati kutokana
na utandawazi uliopo kwa sasa
ndani ya nchi zilizoendelea
Akizungumza
jijini hapa na waandishi wa habari
mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya mkutano
wa benki
ya AFDB kwa mwaka 2012 Bw Ngosha Magonya
ambapo alisema
kuwa mkutano huo
utakuwa na faida kubwa sana
Alifafanua kuwa
kupitia mkutano huo ambao utaanza
Jumatatu ijayo utakuwa na faida kubwa sana
kwa
jiji la Arusha kwa kuwa hata kiwango cha uchumi
kitaaimarika sana kwa kuwa
wageni mbalimbali
kutoka katika maeneo ya nchi mbalimbali
duniani
watabadilishana hata uzoefu
“kwa kipindi
hiki ambacho kuna mikutano ndani ya jiji la
Arusha tunatarajia kuwepo na
utoafuti wa khali ya juu
sana hasa katika mchakato wa uchumi na kwa hali hii
pia
tunatarajia hata kufanya maendeleo mbalimbali ikiwemo
kufanya
marekebisho kwa jengo la kimataifa la AICC”
alisema bw Magonya
Katika hatua
nyingine alifafanua kuwa mbali na kuweza
kuimarisha uchumi wa mkoa wa Arusha
pia wanatarajia
kutumia fursa mbalimbali za kuhakikisha kuwa
wanakutanisha
wafanyabiashara mbalimbali huku
malengo yakiwa ni kuendeleza uchumi
kwa
walengwa.
Pia alifafanua
kuwa mbali na kuweza kuwasaidia
wafanyabiashara hao katika michakato ya kukuza
uchumi pia benki hiyo ina mikakati mbalimbali ya
kuendeleza barabara ambazo
zitaweza kutumika kama
njia ya mawasiliano hapa Tanzania hali ambayo nayo
itachangia kwa kiwango kikubwa sana hata kuimarisha
uchumi wa nchi ya Tanzania
Aliongeza kuwa
hapo awali benki hiyo ilikuwa imeshajenga
barabara ya Arusha –Namanga kwa sasa
ana mpango wa
kujenga barabara ya Arusha – Holile ndani ya Mkoa wa
Kilimanjaro
hali ambayo itachangia sana maendeleo
hasa ya mawasiliano
Alimalizia kwa
kusema kuwa wafanyabiashara hasa
wa mkoa wa Arusha wanatakiwa kuhakikisha kuwa
wanatumia vema fursa za mkutano huo ili kuweza
kuimarisha biashara zao za kila
siku.
|
No comments:
Post a Comment