Shirika la kimataifa la kutetea haki za kibinaadamu,
Amnesty
International, linasema limeambiwa kwamba
Gambia imewanyonga wafungwa tisa kati
ya 47
ambao wamehukumiwa kifo.
Msemaji wa Amnesty, Lisa Sherman Nichols, aliiambia BBC
kwamba wafungwa hao
ni wa mwanzo kunyongwa nchini
Gambia kwa miaka 29, na inasemekana alikuwako
mwanamke
kati yao, na wananchi watatu wa Senegal.
"Tumepata taarifa za kuaminika kuwa watu 9 walinyongwa jana usiku.
Nimezungumza na baadhi ya jamaa zao, ambao
bila ya shaka wako kwenye majonzi,
na wametuomba tuchukue hatua.
Wamegusia kuwa kuna wengine watanyongwa leo usiku.
Tunajaribu kuzitawanya habari hizi ulimwenguni na serikali
ya Gambia inafaa
kujua kuwa macho ya ulimwengu na serikali za
nchi za nje yameelekezwa juu ya
nchi hiyo."
Hapo awali, shirika la raia la nchi hiyo lilimlaumu rais wa
Gambia, Yahya
Jammeh, na lilisema kwamba wengi
waliohukumiwa kifo ni wafungwa wa kisiasa
picha na stori kwa hisani ya bbc
No comments:
Post a Comment