Wanachama
wa klabu ya Yanga, jana kwa kauli moja
walitangaza kuung’oa
madarakani uongozi wa Lloyd Nchunga katika mkutano
uliofanyika
kwenye Uwanja wa Kaunda, jijini Dar es Salaam.
Katika
mkutano ulioratibiwa na Baraza la Wazee kwa
kushirikiana na vijana na kudumu
kwa saa 2 nzima,
ulihamia kwenye uwanja huo kutokana na idadi kubwa ya
wanachama waliojitokeza kuamua hatima ya klabu yao.
Katika
mkutano huo uliodumu kwa saa mbili, kuanzia majira ya
saa 6 hadi 8 mchana, muda
ulivyokuwa ukisogea
, ndivyo wanachama walivyokuwa wanaongezeka.
Ingawa
mkutano huo ulianza na wanachama wapatao 556
, lakini hadi unafungwa, walikuwa
wamefikia 700,
wote kwa pamoja wakiridhia kuuweka
kando uongozi wa Nchunga.
Baada
ya mkutano huo kufunguliwa na dua na sala,
Katibu wa Wazee, Ibrahim Akilimali,
alitoa maneno
machache kuelezea udhaifu wa uongozi wa
Nchunga tangu uingie
madarakani Julai 18, 2010.
Akilimali
aliwaeleza wanachama kuwa, kutokana na
mambo kutokwenda sawa katika klabu yao,
ndiyo maana
waliamua kuchukua jukumu la kuitwaa timu kuelekea mechi ya Simba.
Alisema,
sababu ya wao kufikia hatua hiyo, ni wachezaji kukosa
ari ya kucheza kutokana
na matatizo ya uongozi wa Nchunga
ikiwemo kutolipwa mishahara, hivyo kuishi kwa
dhiki kubwa.
Akilimali
alisema, udhaifu na matatizo ya uongozi wa Nchunga,
yanathibitishwa na wajumbe
wa Kamati ya Utendaji
walioamua kumsusia klabu hiyo.
Alisema,
miezi michache tangu kuingia madarakani, makamu
wake, Davis Mosha alijiuzulu
akifuatiwa na wajumbe wengine wa
Kamati ya Utendaji hivi karibuni, hivyo hafai
kubaki Yanga.
Mbali
ya Mosha, wengine walioachia ngazi, ni Seif Ahmed, Ally Mayay,
Edgar Chibula na
Abdallah Bin Kleb, ambao wote walifanya hivyo
kutokana na matatizo yaliyomo
kwenye uongozi wa Nchunga.
Kuhusu
fedha za kuendesha timu, Akilimali alisema tayari
wameahidiwa kupewa sh mil 750
na watu wenye mapenzi
na klabu hiyo, na kwamba kuna mfanyabiashara mmoja
ameahidi kutoa sh mil 250, hivyo kufikia sh bil 1.
Kati
ya waliopewa nafasi ya kusema machache, ni kipa
wa zamani wa timu hiyo, Hamisi
Kinye na beki Bakari Malima
‘Jembe Ulaya’, ambao waliushutumu uongozi wa
Nchunga kwa usajili mbovu.
Kwa
mujibu wa Katiba ya Yanga, iwapo theluthi ya
wanachama watajiorodhesha na kutia
saini zao,
maamuzi watakayofikia, ni halali.
Baada
ya kupitisha uamuzi huo, Akilimali alisema watawasilisha
orodha ya wanachama
waliojiorodhesha kushiriki mkutano
huo kwa Msajili wa Vyama na Klabu za Michezo
Wilaya ya Ilala kuomba uchaguzi mkuu.
Tangu
Yanga ipoteze mwelekeo wa ubingwa wa Ligi Kuu,
kumekuwa na harakati za kuung’oa
uongozi wa Nchunga
kwa hoja ya kushindwa kazi, huku wachezaji na makocha
wakilia kutolipwa mishahara.
|
No comments:
Post a Comment