contact

husen

Friday, May 18, 2012

MANJI KUINUSURU YANGA

YUSSUF  Manji, ameibuka tena Yanga, baada ya
 kimya cha muda mrefu akijitokeza kwa nia ya
 kuokoa jahazi kutokana hali mbaya ya 
kiuchumi inayoikabili klabu kwa sasa.
Waajiriwa wa Yanga, wakiwemo makocha, wachezaji
 na watendaji hawajalipwa mishahara kwa takriban
 miezi minne, hali inayoashiria uongozi wa klabu hiyo,
 chini ya Mwenyekiti wake, Wakili
 Lloyd Baharagu Nchunga umeelemewa.
  mfanyabiashara kijana anayemiliki mamilioni ya fedha,
 Manji yu tayari kuokoa jahazi kwa kurejesha udhamini katika klabu.
Hata hivyo, ili kurejea kuidhamini Yanga, 
Manji ametoa masharti matano.
Masharti hayo ni; kufanyika uhakiki wa mahesabu
 ya akaunti za Yanga ndani ya siku 90 na wakaguzi
 wa hesabu wa kujitegemea kukagua
 hesabu za kipindi cha kuanzia mwaka 2006 hadi 2012
 kwa ajili ya fedha zilizoingia klabuni.
Sharti la pili ni kuchapishwa magazetini kwa akaunti za 
Yanga siku 15 baada ya kumalizika kwa robo ya mwaka, tatu ni
kuendeshwa zoezi la kura ya maoni ndani ya siku  60
 na kuamua kama wanachama wa Yanga wanataka
 klabu iwe Yanga au la na sharti la nne ni mabadiliko
 ya Katiba ndani ya siku 90.
Kwa mujibu wa barua ya Manji kwa Mwenyekiti wa
 Yanga, Nchunga ameutaka pia uongozi kuidhinisha
 mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa klabu, nafasi
 ambayo iko wazi baada ya Davis Mosha kujiuzulu mwaka jana.
Sharti la mwisho la Manji ni kutaka kufanyika kwa
 Mkutano Mkuu wa wanachama ndani ya siku 30,
 ili kujadili mustakabali wa klabu.

No comments:

Post a Comment