contact

husen

Wednesday, June 27, 2012

KUFUATIA SKENDO YA USAGAJI KAPTENI WA TWIGA STARZ AFUNGUKA

Vyombo mbalimbali vya habari vya Tanzania likiwemo
 gazeti la Mwananchi vimenukuliwa vikiripoti stori
 kwamba Kocha wa timu ya taifa ya Twiga Stars aliejiuzulu
 Boniface Mkwasa alisema moja kati ya mambo
 yaliyomkera Twiga Stars ni wachezaji kadhaa
 kushiriki katika mapenzi ya jinsia moja, wao 
kwa wao kwenye timu.
Nahodha wa timu hiyo 
Sophia Mwasikili amesema “nimefurahi kulizungumzia
 hilo swala kwa sababu limekua likizungumzwa kwenye
 magazeti mengi bila uthibitisho, kocha hakuzungumza
 kwamba kuna vitendo kama hivyo alisema vilikuepo
 kipindi cha nyumba lakini kwa sasa havipo, nimekua 
Twiga Stars toka 2006 mpaka sasa sijaviona hivyo vitendo 
labda mwalimu ndio aliona kwa mchezaji lakini hakuna
 yeyote ambae amewahi kuripoti kwangu”
“Wazazi wetu hawajapenda hili swala, tumedhalilishwa 
na hata kama kuna mchezaji alifukuzwa kutokana na
 hilo basi itakua ni siri kati yake na mwalimu hatujawahi 
kuambiwa, kama Mkwasa atapatikana ni vizuri amtaje
 huyo mtu il iwatanzania wajue lakini kiukweli hakuna
 vitendo kama hivyo Twiga Stars” – Sophia
Exclusive on millardayo.com leo Kocha 
Boniface Mkwasa amesema “sijafanya kikao
 chochote na waandishi wa habari kuzungumzia
 hilo swala na sijazungumza lolote kuhusu ishu ya 
 usagaji nashangaa hawa waandishi wameipata wapi
 hii habari na wanazidi kujenga chuki, ndio maana 
nimekaa kimya wiki nzima sijaongea chochote, na sio
 kwamba nimetoka Twiga Stars ndio nikasema hayo,
 sijawahi kushuhudia hivyo vitu hata siku moja na 
kama vilikuwepo labda ni zamani sana kipindi 
bado hata sijaingia”
Kuhusu kuvipeleka Mahakamani vyombo vya habari 
vilivyoandika hizo habari, Mkwasa amesema 
“mimi sitafanya chochote namwachia
 Mwenyenzi Mungu tu kwa sababu kila mtu
 ana uhuru, ila waandishi wazitumie vizuri kalamu
 zao kwa sababu watasababisha wazazi wasiruhusu
 mabinti zao kuja kucheza kwenye timu ya taifa”

Source millardayo

No comments:

Post a Comment