Kituo
cha ITV kupitia Twitter kimesema mwenyekiti
wa jumuiya ya madakatari Dr.
Stephen Ulimboka
ametekwa na kupigwa na watu wasiojulikana na
anapelekwa katika
hospitali ya mifupa ya Moi.
Dr. Ulimboka ametekwa majira ya saa sita
usiku
na watu watatu waliokuwa na silaha za moto
na kumpeleka kusikojulikana!
Inasemekana
alipigiwa simu na jamaa mmoja
aliyejitambulisha kwa jina moja la
'Abeid' ambaye tangu mwanzo amekuwa
akiwasiliana naye na kujiita afisa wa
serikali
na kudai kuwa alitaka aonane naye
face to face kwa ajili ya
mazungumzo.
Dokta
huyo aliokotwa akiwa na hali
mbaya sana na hawezi kuzungumza.
Tukio
hilo limetokea wakati kumekuwepo
na mgomo wa madaktari nchi nzima ambao
hata
hivyo wameonekana kusalitiana kwa
kutokuwa na msimamo wa pamoja, kwani
maeneo
mengine yote huduma zimeendelea
kama kawaida, isipokuwa katika Hospitali
ya
Taifa ya Muhimbili.
Madaktari
hao wametangaza mgomo usio na
kikomo kwa lengo la kuishinikiza serikali
kutimiza
mahitaji yao, ikiwemo kuboresha mazingira
ya kufanyia kazi pamoja na
kuwapandishia mishahara.
Licha
ya mgomo huo kuanza kuleta madhara
kwa wagonjwa katika siku ya kwanza juzi,
kwa
madaktari kutofanya kazi katika hospitali
mbalimbali nchini, jana hali hiyo
ilikuwa tofauti
kwani sehemu nyingi huduma ziliendelea
kutolewa kama kawaida.
Zitto
Kabwe: Nimesikitishwa sana na habari za
kutekwa, kupigwa na kuumizwa vibaya kwa
Dr. Ulimboka, Kiongozi wa Madaktari nchini.
Ishara mbaya sana.(Twitter)
Source leotainment
No comments:
Post a Comment