contact

husen

Friday, August 17, 2012

ARSENE WENGER AJIPA MOYO

Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesema kitendo ambacho kimefanywa

 na Arsenal cha kumuuza Robin Van Persie kwa klabu ya Manchester United
ilikuwa ni zaidi ya mchezo wa kamari kwani alikuwa mhimili mzuri
 katika klab yake ya hapo awali.
kitendo hicho kimewasononesha sana mashabiki wa arsenal lakini
ukweli ni kwamba  mchezaji anapotaka kuhama klabu kuna mambo
mawili tu ya kufanya. Kumlazimisha kubaki au kumruhusu
 kuondoka na kwenda anapotaka.
Klabu ya Arsenal imepata pigo katika misimu kadhaa mfululizo kwa kuwapoteza
wachezaji kama Cesc Fabregas, Sameer Nasri pamoja na
 Alex Song ambaye yuko mguu nje mguu ndani kusalia kilabuni hapo



Wenger amesema yakwamba anafahamu anakabiliwa na changamoto

 kubwa lakini anaimani yakwamba watazitatua changamoto hizo kwani

Arsenal ni klabu kubwa yenye takribani miaka 125 na kuongeza

 ya kwamba walishapita wachezaji wengi wazuri kilabuni hapo hivyo

anaamini timu yake itakuwa fiti very soon

No comments:

Post a Comment