Mwanamuzi mashuhuri nchini kongo(DRC)
Anton Akgeba Makila Mabe
maarufu pia kama Koffi Olomide aka
Mopao Mokonzi, Aswekwa
lupango na pia kafikishwa kwa Pilato
Mwanamuziki huyo alikamatwa na kufungiwa katika kituo cha polisi
na
kufikishwa mahakamani
jumatano.
Koffi alikamatwa kufuatia vurugu katika hoteli moja mjini
Kinshasa.
Waandishi wa habari wanasema mahakama hiyo ya Kinishasa ilifurika
kutokana na watu wengi kuja kumuona kiongozi huyo wa
bendi ya Quartier Latin akiwa kizimbani.
Kesi hiyo iliharishwa hadi Alhamisi asubuhi wakati
atakaposhitakiwa rasmi.
Wakati wa kesi hiyo hapo jana Koffi Olomide aliwakilishwa na
mawakili 10.
Ugomvi kati ya mwanamuziki huyo na mtayarishi wake Bwana , Diego
Lubaki,
ni kuhusu pesa dola $3,680.
Hakimu alimfahamisha mwanamuziki huyo ikiwa atapatikana na hatia
huenda akafungwa jela miezi sita.
Olomide ni gwiji wa muziki aina ya "soukous", mtindo
ulitokana na jina la kifaransa
"secouer", lenye
maana ya kujitikisa au kujinengua ,
na wachezaji wake vile vile wanatambulika kwa kunengua maungo.
stori kwa na picha kwa hisani ya djchoka.blogspot.com
No comments:
Post a Comment