Alikuwa na umri wa miaka hamsini na
saba na ni mmoja wa
viongozi wenye ushawishi mkubwa na
ambaye utawala
wake ulikumbwa na utata barani
afrika.
Hali yake ya afya imekuwa ikiangaziwa
kwa majuma kadhaa
sasa ingawaje hakukuwa na thibitisho
kuhusu alichokuwa akiugua hasa.
Taarifa ya baraza la mawaziri imesema
kuwa Zenawi alikuwa
akipokea matibabu ng'ambo na afya
yake ilikuwa ikiimarika
lakini akazidiwa siku ya Jumapili
alipolazimika kurejeshwa
hospitali, ''Ingawaje madaktari wake
walifanya kila wawezalo,
alifariki jana mwendo wa 23:40,''
taarifa hiyo imesema
Bwana Zenawi alikuwa kiongozi wa
Ethiopia wakati taifa hilo
lilipoingia vitani na nchi jirani ya
Eritrea mwaka 1998.
Meles Zenawi aliingia mamlakani mwaka
1991 baada ya
mapinduzi lakini akapokea sifa kutoka
kwa mataifa ya magharibi.
Waziri mkuu wa Kenya raila Odinga
ameiambia BBC kuwa
ana hofu kuhusu hali nchini Ethiopia
kufuatia kifo cha Meles Zenawi.
Alisema kuwa hali nchini humo sio
nzuri huku vita vya
kikabila vikiendelea kuwa tishio.
Bwana Odinga alimtaja Zenawi kama
kiongozi mashuhuri
na mwenye elimu bora, aliyejitolea
kuunganisha bara la afrika.
Naibu waziri mkuu Hailemariam
Desalegn anatarajiwa
kuchukua mahala pake.
stori na picha kwa hisani ya bbc
|
No comments:
Post a Comment