Serikali ya Ethiopia imesisitiza kuwa nchi hiyo ni tulivu licha
ya kifo
cha Waziri Mkuu wa nchi hiyo Meles Zenawi aliyekuwa
na umri wa miaka
57.
Zenawi alifariki katika hosipitali katika mji mkuu wa Ubelgiji,
Brussels,
siku ya Jumatatu baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Mwili wake unasafirishwa kuelekea mako makuu ya Ethiopia
Addis Ababa, na
kipindi cha maombolezo ya kitaifa
kimetangazwa nchini humo.
Vyombo vya serikali vimeripoti kuwa Makamu Waziri Mkuu
Hailemariam Desalegn
ndiye atakayeshika madaraka hadi
wakati wa uchaguzi mwaka 2015.
Kifo cha Bwana Zenawi kimezua hofu ya kugombania
madaraka ambayo ingeweza
kuathiri amani ya nchi hiyo.
Ellen Johnson Sirleaf rais wa Liberia amemsifu Bwana Zenawi
kuwa alikuwa
kiongozi mahiri wa kurekebisha uchumi na
pia kiongozi msomi na imara mwenye
ushawishi mkubwa barani Afrika.
Naye waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga awali aliiambia
BBC kuwa ana hofu
kuhusu hali nchini Ethiopia kufuatia kifo
cha Meles Zenawi kutokana na vita vya
kikabila kuendelea kuwa tishio.
Licha ya kuwa kama mmoja wa viongozi wenye ushawishi
mkubwa barani Afrika,
lakini utawala wake ulikumbwa na utata barani humo.
Hali yake ya afya imekuwa ikiangaziwa kwa majuma kadhaa
kabla ya kifo chake
ingawaje hakukuwa na thibitisho kuhusu
alichokuwa akiugua hasa.
Taarifa ya baraza la mawaziri imesema kuwa Zenawi alikuwa
akipokea matibabu
ng'ambo na afya yake ilikuwa ikiimarika
lakini akazidiwa siku ya Jumapili
alipolazimika kurejeshwa
hospitalini. Ingawaje madaktari wake walifanya kila
wawezalo,
alifariki siku ya Jumatatu usiku majira ya saa tano na nusu usiku.
Bwana Zenawi alikuwa kiongozi wa Ethiopia wakati taifa hilo
lilipoingia
vitani na nchi jirani ya Eritrea mwaka 1998.
Meles Zenawi aliingia mamlakani mwaka 1991 baada ya mapinduzi
lakini akapokea
sifa kutoka kwa mataifa ya magharibi.
picha na stori kwa hisani ya bbc
No comments:
Post a Comment