contact

husen

Saturday, May 26, 2012

SIMBA, MAZEMBE NA APR KUMUENZI MAFISANGO

Mabingwa wa  soka Tanzania bara Simba Sports Club 
aka Mnyama kwa kushirikiana na klabu za
 Tp Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
 Congo DRC  pamoja na APR ya Rwanda, zipo katika
 mchakato wa kuandaa mechi maalum kwa ajili
 ya kumuenzi aliyekuwa mchezaji wao, 
Patrick Mutesa Mafisango.
Mafisango ambaye alifariki dunia wiki iliyopita jijini 
Dar es Salaam kwa ajali ya gari alizikwa nyumbani
 kwao Kinshasa, Congo.
Makamu Mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange 
 amesema jana kwamba, hawana budi kumuenzi
 mchezaji huyo kutokana na kutoa mchango mkubwa
 kwa timu hizo enzi za uhai wake.
Aliongeza kuwa fedha zitakazopatikana zitapelekwa
 katika familia ya Mafisango ili ziweze kusaidia wake 
na watoto wake.
Aidha, Simba imezishukuru timu za Yanga
 kupitia wazee
 wa baraza, Azam Fc, Coastal Union,
 Villa Squad ,
 kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom na
 Kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya
 Kilimanjaro kwa michango yao ya hali na 
mali baada ya kutokea kwa msiba huo.

No comments:

Post a Comment