contact

husen

Monday, June 25, 2012

GRANADE LALIPUKA HUKO MOMBASA KABLA YA KUMALIZIKA KWA MECHI YA ENGLAND VS ITALLY

Idadi ya waliopoteza maisha kutokana na bomu lililolipuka
 kwenye baa moja Mombasa Kenya imefikia watatu
 kwa mujibu wa shirika la msalaba mwekundu ambapo
 wawili walifariki dunia wakiwa hospitali.

 Mlupuko huo umetokea Jericho Beer Garden umbali wa
 kilomita saba kutoka kwenye mji wa Mombasa siku moja
 tu baada ya ubalozi wa Marekani Kenya kuonya
 kutokea kwa mlipuko huo, Standard Media Kenya 
wameripoti kwamba wengi wa watu hao walikua wanatazama
 mechi ya England na Italy.
Msemaji wa polisi amesema mlipuko ulitokea kwenye mida
 ya saa nne usiku wa kuamkia leo ambapo wengi wa waliojeruhiwa
 walikua nje ya baa hiyo huku shuhuda wa tukio hilo akisema
 mmoja wa waliofariki alikua kwenye dancing floor.
Inaaminika shambulio hilo linaweza kuwa limefanywa na
 kikundi cha wanamgambo cha Al Shabaab cha Somalia toka


 Kenya ilipotangaza nacho vita october mwaka jana.







No comments:

Post a Comment