contact

husen

Monday, June 11, 2012

HERMY B AFUNGUKA JUU YA KILICHOTOKEA KATI YAKE NA AY

Tarehe 23/05/2012 tuliandika makala inayosema:
 ‘Ay na B’Hits na urafiki uliochuja kimya kimya’. 
Makala hiyo ilijaribu kuangalia uhusiano wa
 Ambwene Yesaya na Hermy B ambaye ni
 producer na mwenyekiti mtendaji katika kampuni
ya B’Hits Music Group.

Hermy B ambaye ameisoma makala hiyo, ametuandikia 
barua kukanusha baadhi ya mambo tuliyoyaandika
 na pia kutoa ufafanuzi wa namna mambo
 yalivyokuwa na yalivyo sasa:

Ningependa kujibu shutuma zilizoandikwa na
 blog yako kuhusu uhusiano wangu na swahiba
 wangu A.Y. Ningependa ifahamike kwamba
 mimi na A.Y  kwa kipindi cha miaka 4 tumefanya
 kazi za muziki kwa karibu pamoja na kazi
 nyingine za biashara.  Ni kawaida na inaeleweka
 kwamba mahali popote watu wanapofanya
 kazi pamoja kugongana katika mawazo au
 lugha ni jambo la kawaida, na ndio changamoto
 zenyewe. Si jambo la ajabu kama mimi na
 swahiba wangu A.Y. kupishana katika kazi.




Baada ya kusoma makala inayonihusu kwenye blog
 yako nimeona ni umuhimu wa kujibu ni makala yako 
haswa kuhusu swali linalohusu utu na tamaa ya pesa.
 Kwanza ningependa ieleweke kwamba
 umeniweka katika picha ya mtu mwenye 
tamaa kubwa ya pesa na nisiejali utu picha
 amabayo imeanza kunisumbua katika shuhuli
 zangu kwa muda mfupi tu kwani wananchi
 wameanza kuniona hivyo.

Hivyo  nimeona ni lazima nijibu kwani nikiiacha
 bila kujibu madhara yake yatakuwa  mabaya. 
 Kwanza napenda uelewe sijawahi kuwa msimamizi
 wa kazi za A.Y zaidi ya kuwa producer wa
 nyimbo zake tu. Kipindi chote hicho nimekua
 natumia utaalamu wangu kwenye kutengeneza
 tu muziki wake. Maswala mengine yoooote
 amekuwa akifanya mwenyewe tena
 bila msaidizi.

Pia ufahamu bila A.Y na MwanaFA kunipa nafasi
 kutengeneza muziki wao nisingekua hapa nilipo.
 Nadhani inaeleweka mahali popote duniani kwamba
 kipaji ili kifahamike kwa watu lazima kipitie
 kwa mtu fulani au mkondo fulani. Si ajabu
 kama kipaji changu cha kuproduce muziki
 kimeweza kufahamika kwa kupitia kwa A.Y.
 Mimi sio mungu labda ningekua sehemu nyingine
 na mafanikio makubwa zaidi au machache zaidi,
lakini nachojua rafiki yangu amenipa ngazi ya
 kufika huku nilipo sasa, sijawahi kuficha hilo
 na hata wao wenyewe wanajua na bado
 nashukuru kwa hilo.

A.Y hajawahi kuingia mkataba wa aina yoyote
 na kampuni ya BHits Music Group Limited wala
 mimi binafsi uliombana kufanya kazi na mimi na
 sio mtu mwingine yoyote. Nimetengeneza
 nyimbo zisizopungua 30 za A.Y, kwa ajili ya
 albamu yake katika kipindi cha mwaka 
2008 mpaka 2011. Baadhi ya nyimbo hizo 
zimeshatoka na nyingine bado zipo zikisubiri
 uhitaji wake. Wote tulikua na lengo la kutengeneza
 muziki kwa wingi na kuuza kwenye soko zuri la
 muziki ili tufaidike kwa pamoja.

Muda wote muziki ulikua unatolewa na unafanya
 vizuri kwa radio na T.V na show zilikua zinafanyika
 na zote nilikua nazijua iwe ndani ya nchi au
 nje ya nchi hii  hata malipo nilikua nafahamu
 ni kiasi gani na sijawahi kufichwa na A.Y kuhusu hilo.

Utata umekuja kwenye malipo yaliyotajwa kwenye
 blog yako ambayo yameniudhi sana na baadhi ya
 wasanii wanaopenda kurekodi kwangu wameanza
 kuwasiliana na mimi kuuliza bei imepanda lini na
 kama inawahusu pia.

Kutoelewana kwetu kwetu kibiashara ilikuwa mwezi
 February mwaka huu yakihusu malipo ya album hiyo.
 Baada ya hapo niliamua kufunga mdomo wangu na
 nisingesema chochote kwani haya yalikua yananihusu
 mimi na rafiki yangu tu. Nimeamua kuongea
 sasa kwani nahisi nimeshambuliwa kwa 
mara ya pili kuhusu makubaliano haya na mara
 ya kwanza niliamua kukaa kimya.

Kwanza nataka ufahamu Katika kipindi cha kutokea
 2008 mpaka leo hii (miaka 4) kwa matumizi ya
 nyimbo hizo, ambazo amekwishafanyia show
 nje na ndani ya nchi na nyingine kumpatia
 nominations na tuzo tofauti, nilichowahi kulipwa
 hakitaweza kuzidi shilingi milioni tatu kwa
 malipo ya awamu tofauti kwa miaka minne.
 Kilichotokea ni kwamba, mwaka huu mwanzoni
 kabisa, A.Y aliwasiliana na mimi akiwa na
 mipango ya kuzindua albamu yake. Na alitaka
 kuzinunua zile nyimbo kutoka kwangu akiwa na
 mpango mpya wa kuiuza albamu kwa mpango
 wake binafsi pasi na mimi. Nilishindwa kuelewa
 nini anakifanya hasa alipoomba alipie wimbo
 mmoja mmoja tena kwa bei ya msanii wa
 kawaida anaehangaika kutoka.

Niliamua kukubali kwamba ameamua kufanya
 hivyo na sina nguvu ya kumzuia basi nikajaribu
 kupata malipo halisi ya kazi yangu. Ubishi wangu
 ulikua kwamba msanii mdogo hawezi kulipa bei
 sawa ya kurekodi na msanii mkubwa, kwani 
hata malipo ya msanii mkubwa na mdogo baada
 ya kazi yoyote iwe ya matangazo ama show huwa
 hayafanani. Bei niliyotaja haikua millioni kumi,
 ni uongo mtupu na kwa wimbo mmoja
 niliomba nilipwe millioni 2.

Akakubali kwa bei hiyo ya Millioni 2 japo
 nilihisi hakuridhika kabisa. Nilimtumia mkataba
 wa makubaliano yetu ambayo kweli baadae 
aliona kwamba bei hiyo kwake ni kubwa sana
 hivyo hatukusaini makubaliano. Tulibadilishana
 meseji kwa simu kwa muda mrefu sana na
 niliona biashara hii itavunja urafiki wetu.

Nilifikiria sana kwamba nyimbo hizi nimekaa
 nazo toka 2008 bila kuingiza chochote na
 maisha yanaenda pia. Sikuona sababu ya kuharibu
 urafiki wetu wa muda mrefu kwa mabishano haya.
 Kwa Ujumbe wa simu nilimueleza A.Y
 anakaribishwa aje achukue nyimbo zoooooote
 anazohitaji kwa albamu yake BURE (bila malipo).
Lakini nilimuomba anisamehe sitomix zile ambazo 
bado hazijamixiwa, ila ampatie producer
 mwingine amfanyie hiyo kazi.

 Mpaka naona hii makala A.Y hajaja kuchukua
 hizo nyimbo na ndio naelewa kua hayupo na
 BHits tena na wala taarifa zote hizo mbili
 hajawahi kunipatia. Huu ndio ukweli halisi.

Swala la mimi kuwa na wivu na kinyongo na
 mafanikio ya A.Y ni uongo na nashangaa umetoa
 wapi maneno hayo. Kama kulipwa kidogo,
 huku nikiona A.Y anaingiza fedha nyingi
 kwa muziki tunaotengeneza pamoja basi
 ningekua nimegombana nae toka mwaka
 2009 labda.

Narudia kwamba nilikua najua kila show yake
 inapofanywa na sikuwahi kujisikia vibaya.
 Nataka utambue pia nilikua na akili timamu
 wakati nafanya kazi na A.Y na muda wowote
 nilikua na uwezo wa kubadili mawazo na
 kutaka tuandike makubaliano kwa karatasi
 ila sikufanya hivyo na wala sijutii chochote
 kwa utaratibu wetu wa hatari wa kufanya kazi
 bila mkataba wa maandishi na ndio maana nipo
 radhi hata sasa kumpatia nyimbo hizo bure
 kama nlivomwambia hapo mwanzo. Nina meseji
 zote na email za mazungumzo yetu ambazo
 nilihifadhi nikijua ipo siku nitaonekana mimi
 ndie mkorofi, hivyo nachokisema nina
 hakika nacho asilimia 100.

Picha nyingine mbaya ulioichora ni kujaribu
 kuonyesha kuna kutopendana kati ya
 maproducer. Mimi Master Jay na Marco Chali
 ni marafiki wazuri tu na mpaka leo hii nikiwa
 na shida na nikamhitaji Marco Chali au Master
 Jay nitampigia simu bila aibu kwani hakuna
 ugomvi kati yetu. A.Y, Master Jay na Marco
 Chali pia ni marafiki wa siku nyingi na katika
 kipindi cha miaka minne akiwa Bhits kwa
 hiari yake na sio mkataba, A.Y amekuwa
 akienda MJ records anapojiskia na mara kadhaa
 mimi nimeenda na A.Y na mara kadhaa
 nimeenda peke yangu tena kwa ajili ya
 shughuli zangu binafsi.

Pia ufahamu katika kipindi hicho A.Y alikua 
akitumia muda mwingi MJ Records kuliko
 Bhits na hiyo yote ilikua ni mipango yake
 binafsi. A.Y hajawahi kuzuiwa kufanya kazi
 na mtu mwingine kwani ni msanii huru.

Ndugu yangu mimi ni mtu mpole nisiye na
 ugomvi na mtu hapa mjini. Nasikitika sana
 kwa jinsi kwenye makala yako ulivyojitahidi
 kuonyesha kwamba mimi na swahiba wangu
 tumejenga uadui. 

Wasalaam
Hermes Bariki Joachim (Hermy B)
Managing Director

Source leotainment

No comments:

Post a Comment