contact

husen

Saturday, June 23, 2012

JOH MAKINI ATETA


Joh Makini amerudi kwa kishindo na ngoma yake 
iitwayo Manuva na iliyotengenezwa na mtayarishaji
 mkongwe Ambrose aka Dunga.

Tumepiga story na Joh Makini aka Mwamba
 wa kaskazini kuhusu masuala mawili
 matatu kama ifuatavyo.

Kuhusu wapi aliporekodi Manuva, anapoishi na 
anachofanya producer Dunga

Manuva tumeifanyia pale kwa Dunga nyumbani  ana 
microphone yake, amegonga beat nyumbani ana
 monitors (speaker) kwahiyo tukafanya pale, 
halafu tukaenda kufanya final mixing na 
mastering kwenye studio za B’Hits kwa 
Hermy B. Dunga anaishi Mikocheni. Anafanya
 production na kazi zake binafsi.

Kuhusu wasanii wa Hip hop kutopiga show 
za hela kama wanazofanya wasanii wa kuimba
 kama Diamond

Mimi nafikiri hiyo ni kwa wadau tu ambao industry
 wanaiona hivyo lakini kwa upande mwingine
 nafikiri watu wa hip hop pia wengi wako smart
 sana kibiashara na watu wenye misimamo
 mara nyingi,  sasa hiyo kwenye industry inakuwa
 kama shida fulani hivi.

Kuhusu mipango ya Weusi

Weusi tuna hii albam yetu ya pamoja ya Weusi,
 baada ya hapo kila mtu anaenda solo sasa, lakini
 kampuni inabaki pale pale kufanya biashara za
 Weusi kama kuuza nguo za Weusi na cds.

Kuhusu kama biashara hizo zinawalipa

Yeah inatulipa, faida ipo kwasababu tunanunua bidhaa, tunaitengeneza,tunauza kwa kiasi fulani cha
 hela ambacho kina faida pale juu yake, na sio
 mbaya inatusaidia kidogo mafuta ya gari na 
vitu vidogo vidogo kuendesha maisha. Sisi 
t-shirt zetu tunaziuza kwenye maduka ya watu
 tu yaani kama Born 2 Shine, kwa CP jembe pale
 Mwenge kwahiyo tuna washkaji zetu wenye
 maduka, tukitoa mzigo tunawapelekea kwenye
 maduka yao kwasababu nao wanapenda
 kusupport hip hop, kwahiyo tunafanya nao 
biashara kwa style hiyo.


Kuhusu kitu asichokipenda kwenye muziki wa sasa

Upigwaji wa nyimbo kwenye radio stations, nyimbo 
zinakuwa hazidumu. Wimbo unatolewa, unapigwa 
wiki,unapigwa wiki inayofuata wiki nyingine
 zinakuwa hazipigwi tena. Yaani hakuna upigwaji
 ambao unaweza kuufanya wimbo uishi. Kuna
 ngoma kama za Hip hop usipozipiga mara nyingi
 watu hawawezi kuelewa sababu utakuta kuna
 metaphors,mle ndani kuna mashairi magumu,
 mtu anatakiwa ayasikike mara mbili, mara tatu
 ili aweze kuyatafakari na kuyaelewa. Nadhani
 tunahiji airtime nzuri kwaajili ya watu kuelewa 
hiki tunachokuwa tunakiongea kwenye mistari yetu
 tofauti na wasanii wengine wa kuimba sababu wao
 muziki wao unategemea tu melody sio katika uandishi.
 Kwahiyo watu wakishapenda melody basi wimbo
 unahit lakini wimbo wa hip hop kama watu
 hawajaelewa maishairi inakuwa kidogo kazi.


SOURCE LEOTAINMENT

No comments:

Post a Comment