contact

husen

Thursday, June 21, 2012

KANUMBA KUENZIWA MAONYESHO YA SABA SABA

Bado mpaka sasa kumbukumbu za watanzania hazijalala, movie star

 marehemu Steven Kanumba bado anakumbukwa kwa sababu bado kazi zake

 nyingi alizozifanya zinaendelea kuonekana katika maisha ya kila

 siku ya watanzania wengi.

Wakati huu ambapo maonyesho ya sabasaba yanakaribia kuanza 

Dar es salaam familia yake imeamua kuchukua banda maalum

 kwenye viwanja vya saba saba kwa ajili tu ya kuendelea

 kumuenzi Marehemu Kanumba.


Seth ambae ni Mdogo wake waliekua wakiishi pamoja

 Sinza Dar es salaam amesema ni banda la Kanumba litakalokua

 na Nguo zenye alama alizokua anazitumia Kanumba ikiwa ni 

pamoja na jina na ujumbe, kutakua na picha zilizo kwenye frame za 

Kanumba zinazomuonyesha toka akiwa utotoni, pia vikombe, kanga

, bazee na vitu vingine vingi vyenye alama na picha za Kanumba.

Seth amesema Mama mzazi wa Kanumba pamoja na watu aliokua

 akifanya nao kazi Kanumba watakuwepo kutoa maelezo

 mbalimbali kuhusu Kanumba na kazi zake.

source millard ayo

No comments:

Post a Comment