contact

husen

Wednesday, June 13, 2012

DOGO JANJA APIGWA CHINI TIP TOP


Nyota wa muziki wa kizazi kipya  kutoka  ‘kruu’ ya  Tip Top 
Connection  yenye maskani yake pande za  Manzese  jijini 
 Dar  es  Salaam  Abdul Abubakar Chende  ‘Dogo  Janja’
  ametupiwa  virago   ndani ya kundi hilo.
Akizumngumza mapema leo kiongozi wa kundi hilo
 Hamad Ally  ‘Madii’  amesema kuwa  Dogo Janja 
 ameshindwa  kuendana na  makubaliano halisi
 yaliyokuwepo baina yake na uongozi wa kundi hilo ikiwemo
  kuhudhuria  shuleni kama alivyokuwa akitakiwa  kufanya
 kila siku  badala yake  amekuwa akiendekeza  starehe na
  wakati mwingine kufanya mambo ambayo kwa namna moja
 ama nyingine yalikuwa yanalichafua kundi hilo.
“Tumemkabidhi kwa kaka yake mapema leo tukiwa  maeneo
 ya Ubungo tayari kwa safari ya  kurudi kwao  na wakati
 huo tulifanya mawasiliano na baba yake  kumuarifu kuwa
 Tip Top   hatuko na mwanae kwa sasa”  alisema Madii
Katika hatua nyingine Madii  amesema kuwa Dogo Janja
 alilewa sifa na  kujisahau kufanya yale anayotakiwa kufanya
 ndani nanje ya kundi  kufuatia mafanikio ya muziki aliyoyapata
 akiwa  na Tip Top Connection kwani hivi karibuni alitega
 shule na kwenda kujificha  nyumbani kwa TundaMan
  hukua akimuaga Madii kuwa anakwenda shule.
Kuona hivyo TundaMan aliamaua kumuarifu Madii na
 mara moja  kiongozi huyo wa kundi aliamua kwenda
  kumsaka,  lakini baada ya dogo Janja kugundua kuwa
 Madii anakuja aliamua kukimbia na kwenda kujificha 
 uchochoroni lakini akiwa huko mafichoni bahati mabaya  
alikanyaga  kuku  na  siri yake kujulikana kuwa amejificha
 hapao ndipo alipokamatwa na kuamriwa kufungasha kilicho
 chake  tayari kurejea ‘kileji’. vimekuwa ni vitendo vya 
kila mara kukacha kuhudhuria shule, tumechoka na 
hatukuwa na njia nyingine ya kufanya alisema Madii'

SOURCE TEEN TZ

No comments:

Post a Comment