contact

husen

Tuesday, June 26, 2012

WADAU WALIA NA KIINGEREZA, UZUNGU KWENYE FILAMU ZA KITANZANIA

Msanii wa filamu ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kituo cha
 Mafunzo ya Filamu cha Tanzania Film Training Centre (TFTC)
 Emmanuel Myamba maarufu kama Pastor Myamba akiwasilisha 
mada kwenye Jukwaa la Sanaa wiki hii. Kushoto kwake ni Katibu
 wa Shirikisho la Filamu nchini Wilson Makubi

Na Mwandishi Wetu


Wadau wa Sanaa wamehoji uhalali wa wasanii wa filamu kutumia
 kiingereza kwenye majina ya filamu zao huku wakishangazwa na 
kazi hizo kubeba maudhui ya kizungu zaidi.


Wakizungumza wiki hii kwa nyakati tofauti 
kwenye programu
 ya Jukwaa la Sanaa, wadau hao walishangazwa 
kitendo cha filamu
 hizo kutumia majina ya kizungu
 wakati hapa kwetu kuna filamu
 nyingi kutoka nje zinazotumia lugha
 za kihindi, kichina, kifaransa 
 na zinafanya vizuri.


“Hoja kwamba, wanatumia majina ya kiingereza ili kuteka soko la
 kimataifa ni ya kitoto, mbona hapa kwetu kuna filamu nyingi
 za kihindi na kichina zinanunuliwa kwa wingi? Hapa kuna udhaifu 
katika kutengeneza filamu zenye ubora tujikite huko”alisema 
Mzee Nkwama Bhallanga.


Kwa mujibu wa wadau wengi waliozungumza,
 filamu ni taaluma 
inayozungumza kwa kutumia picha na 
vitendo zaidi hivyo haihitaji
 mtazamaji kufahamu lugha iliyotumiwa
 ili afahamu maudhui na ujumbe
 unaowasilishwa na kazi husika ya filamu.


“Maneno kwenye filamu si muhimu
 sana, kinachozungumza
 ni matendo
 na picha zaidi, ndiyo maana kuna watu wanaangalia
 picha za Kikorea na 
 wanaburudika na kuelewa kinachoendelea”
 alisema Godfrey Lebejo
 ambaye ni Murugenzi wa Idara ya Utafiti, Mafunzo
 na habari, BASATA.


Aliongeza kuwa, kinachoitesa tasnia ya filamu kwa 
sasa ni kukosekana kwa weledi na uhalisia wa
 tamaduni zetu kunakosababishwa na wimbi kubwa
 la watu kujiingiza kwenye filamu ili kufanikisha
 mambo yao yaliyo nje ya maadili na utamaduni wetu.


“Inawezekana vipi utengeneze filamu ambayo baba,
 mama na watoto hawawezi kukaa pamoja kuitazama?
 Tufike mahali tuseme mambo haya ya kipuuzi
 basi kwenye filamu zetu” alionya Lebejo.


Awali akiwasilisha mada kuhusu Filamu, wasanii
 na haja ya kujiendeleza kielimu, Msanii wa
 filamu Emmanuel Myamba maarufu kam
 Pastor Myamba alisema kuwa, tasnia ya
 filamu inakosa weledi hivyo
 kuhitaji mabadiliko.


“Ni wazi ukiangalia filamu zetu zinakosa weledi katika
 uandishi wa miswada, uongozaji, uhariri na hata
 uumbaji wa wahusika. Lazima tukubali udhaifu huu
 turekebishe” alisema Myamba ambaye kwa sasa
 amefungua kituo cha mafunzo ya filamu kiitwacho 
Tanzania Film Training Centre (TFTC)
 kilichoko Ubungo.
 
SOURCE DJ CHOKA

No comments:

Post a Comment