contact

husen

Sunday, August 26, 2012

GAMBIA YAANZA KUNYONGA WAFUNGWA

Rais wa Gambia, Yahya Jamme
Shirika la kimataifa la kutetea haki za kibinaadamu,
Amnesty International, linasema limeambiwa kwamba
 Gambia imewanyonga wafungwa tisa kati ya 47
 ambao wamehukumiwa kifo.
Msemaji wa Amnesty, Lisa Sherman Nichols, aliiambia BBC
 kwamba wafungwa hao ni wa mwanzo kunyongwa nchini
 Gambia kwa miaka 29, na inasemekana alikuwako mwanamke
 kati yao, na wananchi watatu wa Senegal.
"Tumepata taarifa za kuaminika kuwa watu 9 walinyongwa jana usiku.
Nimezungumza na baadhi ya jamaa zao, ambao
 bila ya shaka wako kwenye majonzi, na wametuomba tuchukue hatua.
Wamegusia kuwa kuna wengine watanyongwa leo usiku.
Tunajaribu kuzitawanya habari hizi ulimwenguni na serikali
 ya Gambia inafaa kujua kuwa macho ya ulimwengu na serikali za
 nchi za nje yameelekezwa juu ya nchi hiyo."
Hapo awali, shirika la raia la nchi hiyo lilimlaumu rais wa
 Gambia, Yahya Jammeh, na lilisema kwamba wengi
waliohukumiwa kifo ni wafungwa wa kisiasa
 
picha na stori kwa hisani ya bbc

No comments:

Post a Comment