contact

husen

Monday, August 27, 2012

KIFO CHA ABOUD ROGO CHASABABISHA VURUGU MOMBASA

 
Ghasia zimezuka mjini Mombasa baada ya mhubiri wa kiisilamu ambaye
 pia alikuwa mshukiwa wa kufadhili kundi la wanamgambo la
 Al shabaab nchini Somalia, Aboud Rogo, kuuawa kwa kupigwa
 risasi mjini Mombasa pwani mwa Kenya.
Mtu mmoja inaarifiwa ameuawa na wengine kujeruhiwa
 katika mtaa wa Mejengo kufuatia makabiliano kati ya polisi
 na mamia ya watu walioghadhabishwa na kitendo cha kuuawa
 kwa bwana Rogo ambaye alikuwa mhubiri wa kiisilamu mjini Mombasa
Hali ingali tete wenye maduka wakilazimika kuyafunga
 maduka yao na watu kukimbilia usalama wao katika mtaa
 wa Majengo katika maeneo ya kati ya mjini Mombasa.
Inaarifiwa Aboud Rogo,alipigwa risasi asubihi ya leo na
 kuaawa wakati alipokuwa akimpeleka mke wake hospitalini
 katika mtaa wa Bamburi mjini Mombasa.Watu wamechoma
 magari na hata kuvamia maduka huku hali ya wasiwasi
ikitanda polisi nai wakifanya kila hali kuweza kutuliza mambo.
Duru zinaarifu kuwa huenda Rogo aliuawa na polisi
 ingawa ripotio hizi bado hazijathibitishwa.
 
Anasemekana alipigwa risasi akiwa ndani ya gari lake
 ambalo lilikuwa limewabeba watu wengine sita,
alizikwa baadaye saa za mchana.
Vile vile Rogo alikuwa anakabiliwa ka kesi ya umiliki haramu
 wa silaha ambapo polisi walidai kuwa alikuwa na njama ya
 kushambulia kanisa moja la kikatoliki mjini humo.
Aboud Rogo Mohammed alikuwa kwenye orodha ya
 Marekani na ile ya Umoja wa mataifa ya watu wanaosaidia
katika harakati za kundi la wanamgambo wa kiisilamu nchini
 Somalia la al-Shabab
Kulingana na ripoti ya umoja wa mataifa, Rogo alisaidia kundi la
 al-Shabab kusajili makurutu wapya. Pia alikuwa anakabiliwa na
 madai ya njama ya mashambulizi dhidi ya kanisa moja mjini Mombasa.
Kwa mujibu wa taarifa, bwana Rogo alipigwa risasi wakati
 akiendesha gari lake katika mtaa a Bamburi mjini humo.
Aboud Rogo Mohammed aliwekwa nwenye oriodha ya
 Marekani ya watu waliowekewa vikwazo mwezi Jilai,kwa
 kujihihusisha vitendo vyinavyohujumu amani na usalama nchini Somalia.

Wapiganaji wa al Shabaab

Baraza la usalama la umoja wa mataifa lilimwekea vikwazo
 vya usafiri na pia kupiga tanji mali zake mwezi Julai, wakisema
 kuwa alitoa ufadhili wa kifedha, usafiri na kusaidia kundi
 hilo kwa vifaa vya kisasa.
Ilimtuhumu kwa kuwa kiongozi maalum wa vuguvugu la
 al- Hijra nchini Kenya ambao pia wanajulikana kama
 Muslim Youth Center, ambalo linatazamiwa na wengi
  kama lililo na uhusiano wa karibu na al-Shabab.
Umoja wa mataifa ulisema kuwa bwana Rogo alitumia kundi
 hilo kama njia moja ya kuwatia watu kasumba ya siasa kali hasa
 wanaoongea lugha ya kiswahili kwa lengo la kufanya
 mashambulizi ya kigaidi.
 
picha na stori kwa hisani ya bbc

No comments:

Post a Comment