contact

husen

Thursday, September 6, 2012

MANECK AMCHANA DOGO JANJA

Producer Maneck ambae ni mshindi wa tuzo kwenye KTMA 2012
 ameamua kuzungumza ya moyoni kwa kuijibu kauli Dogo Janja
 aliyoitoa kwamba Producer huyo kauponda uwezo wa Marco Chali.
Ishu ilianza wakiwa club Maisha Dar es salaam jumapili
 iliyopita ambapo Dogo Janja anadai alikwenda sehemu ya
 V.I.P na kumsalimia Maneck ambae hakujibu salamu ila
 aliporomosha matusi mazito kwa Dogo Janja pamoja na
 kumpiga biti kwamba asimsogelee.
Baada ya hapo Dogo Janja akashuka chini kwenda
 kumwita meneja wake wa WATANASHATI ambae
ni Ostaz Juma ambapo kwa maelezo ya Dogo Janja, Maneck
 alianza kuiponda single mpya ya Dogo Janja na PNC
 waliyoirekodi kwa Marco Chali ambayo mwanzoni ilikua
 irekodiwe kwa Maneck alieiponda kwa kusema ni ya kawaida
 sana kwa sababu imefanywa na Marco Chali.
Jibu alilolitoa Maneck baada ya kusikia kwamba Dogo Janja
 amenukuliwa kwa hayo maneno, namkariri akisema
“ndio ninavyokwambia sitakagi watu masnich kama huyo,
Marco Chali ni mtu ambae namfil sana anafanya kazi nzuri,
 siwezi kuongea kitu kibaya kwa Marco kwa sababu leo na
kesho nitamfata nitamuomba msaada wa kitu chochote kile
 hata material sasa nitawezaji kusema hivyo kwa mfano sasa,
Dogo Janja ni mtu ambae anataka tu kufanyaga vitu watu
wapishane kauli mambo ya kijinga ni utoto akikua nadhani
 ataacha hizo tabia zake, na ndio maana nikamwambia kaa
 mbali sitaki uongee na mimi that’s all”

No comments:

Post a Comment