contact

husen

Thursday, April 11, 2013

MZEE MAANDELA ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALI


Rais mstaafu wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, 
ameruhusiwa kutoka hospitali ambako akitibiwa homa
 ya mapafu yaani pneumonia kwa siku kumi.

                                       Serikali imetoa taarifa kusema kuwa hali ya Bwana Mandela, 
mwenye umri wa miaka 94, imetengenea sana na ataendelea
 kutibiwa nyumbani.
Hali ya Bwana Mandela ilishtusha mwezi Disemba mwaka
 jana ambapo alilazwa hospitali kwa karibu majuma matatu kwa 
sababu ya ugonjwa wa mapafu na kijiwe kwenye nyongo.
Rais Zuma aliwashukuru matabibu na wauguzi kwa jitihada yao ya 
kumuungalia Bwana Mandela kwa uzuri.

No comments:

Post a Comment