contact

husen

Monday, June 4, 2012

HOPE FOR TANZANIA WATOA MSAADA WENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 15


Shirika lisilo la kiserikali la Hope For Tanzania limetoa computer 92
 zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 15 kama 
mchango wa kuinua kiwango cha elimu katika
 shule nne jijini Arusha.
 Wakurugenzi wa shirika hilo hapa Tanzania Felex Masenge
  na Naomi Masenge wamesema kuwa msaada huo
 unatokana na wafadhili wa shule isiyo ya kiserikali ya
 Tuishime ambao waliahidi kuzisaidia shule 10 jijini
 arusha vifaa hivyo  ili wanafunzi waweze
 kujifunza somo la Tehama.
Felex amesema kuwa zoezi hilo la kupatiwa computer 
 linaendelea hali ambayo itatoa fursa kwa shule
 hizo kufanya vizuri kielimu katika ulimwengu
 wa sasa wa sayansi na teknolojia.
Akikabidhi computer  hizo kwa wakuu wa shule
 hizo ambazo ni shule ya msingi uhuru,ukombozi
,kijenge na tuishime mgeni rasmi  katika  hafla hiyo 
Afisa elimu vielelezo Godfrey Augustino amesema
 kuwa vifaa hivyo vimekuja wakati muafaka na
 amewataka kuvilinda na kuvitunza vizuri.
Pia amesema kuwa shule nyingi za serikali zinakabiliwa
 na changamoto ya ukosefu wa fedha  hali ambayo
 inapelekea kushindwa  kununua computer  na wanafunzi
 kushindwa kufanya mitihani ya Tehama kama ilivyo
 kwa  shule  zinazomilikiwa na watu binafsi.
Aidha Augustino ametoa wito kwa wakuu hao wa
 shule kuzitunza na kuzilinda  na kuwa hatokuwa
 tayari kupokea taarifa ya  kupotea ama kuibiwa 
kwa vifaa hivyo   bali hatua kali za kisheria
 zitachuliwa dhidi ya mwalimu husika.
Lakini hata hivyo amewataka walimu kwenda
 shule na kwenda kujifunza alimu ya computer ili
 waweze kuwafundisha wanafunzi somo hilo la Tehama
 na hatimaye waweze kufanya vizuri katika mitihani yao.
Akionge kwa niaba ya wakuu wa shule diwani wa kata ya
 sokon one Michael Kivuyo amesema kuwa ni vyema
 watanzania wakaiga mfano huo kwa kuchangia kuinua
 elimu katika shule za msingi na sio kuchangia ama kutoa
 msaada kwa mambo yasiyo ya msingi katika jamii

No comments:

Post a Comment