Baraza la Sanaa la
Taifa (BASATA) na Tasasi ya Gaba Arts
mapema wiki hii wameendesha semina fupi
kwa
Wasanii wa filamu ili kuwajengea weledi katika
eneo la uandishi bora wa
miswada ya sinema
(script writing).
Semina hiyo
iliyoendeshwa kupitia programu
ya Jukwaa la Sanaa kwenye Ukumbi wa BASATA
ilijikita katika maeneo ya namna ya kuendeleza wazo
hadi sinema ya kusisimua,
namna ya kufikia
hisia za watazamaji,ujenzi mzuri wa matukio,
kutengeneza
wahusika na mfumo wa hadithi, Mwanzo,
kati na hitimisho.
Akitoa mada kwenye
programu hiyo maalum, Mkurugenzi
wa asasi ya Gaba Arts James Gayo alisema kuwa,
muda umefika sasa kwa wasanii wa filamu kusaka
maarifa ili kutengeneza sinema
zenye visa vipya,
zenye weledi na zisizosukumwa na matakwa
au maelekezo ya
wasambazaji.
“Wenzetu kutoka nje
wanatamani sana kupata
vitu kutoka Afrika vyenye kuzungumza uhalisia
wa maisha
ya kwetu, wanataka kuona vitu vipya
hivyo, katika uandishi wa muswada wa sinema
suala
la uhalisia na visa vyenye utofauti ni la msingi sana”
alisisitiza Gayo.
Alizidi kueleza kuwa
watazamaji wa sinema (filamu)
huwa wana kawaida ya kuchoka pale wanapolishwa
visa vya aina moja muda wote na akaonya kuwa
kama wasanii hawatajikita katika
kubuni visa vipya
na vyenye kugusa uhalisia wa maisha yao wadau
watasusia
kununua.
“Ikiwa tutaendelea
kutengeneza filamu zisizo na weledi,
zenye visa vilevile na zenye kusukumwa na
wasambazaji
au haja ya kuchuma fedha za haraka tu watu
watatuchoka na baadaye
soko litakufa” alionya Gayo.
Gayo ambaye amepitia
mafunzo ya utengenezaji
filamu katika mataifa mbalimbali ikiwemo Marekani
alitaja sifa za muswada (script) bora kuwa ni
pamoja na kubeba wazo
linalozalika kwenye jamii,
visa vyenye uhalisia na vipya, utengenezaji mzuri wa
wahusika na sifa zingine nyingi.
Kwa upande wake
msanii wa mashairi Mrisho Mpoto
ambaye alikuwa miongoni mwa waliohudhuria
semina hiyo alisema kuwa, wasanii wa filamu
wanahitaji kusaidiwa kwani kwa sasa
soko la filamu
limekuwa la kitumwa na lenye kuburuzwa na
matakwa ya wasambazaji
bila weledi.
Akihitimisha programu
hiyo, Katibu Mtendaji wa
BASATA Ghonche Materego alishauri wasanii wa
filamu
kujipanga kushirikiana na wasomi wenye weledi
katika maeneo yao ili kuzalisha
kazi zenye weledi la ubora.
E
“Tuna wataalam wengi
katika Sanaa, wamebanana
na mambo mengi lakini ni vema wasanii
tukawatumia na
kushirikiana nao katika kuboresha
kazi zetu” alisisitiza Materego.
source dj choka
No comments:
Post a Comment