Ijumaa ya August 17 2012 na ijumaa nyingine kabla ya hii ya
August 17 zimekua siku mbaya kwa Madame Rita Paulsen
Big boss wa Benchmark Production ambayo ndio muandaji wa
mashindano ya Bongo star search.
August 17 shoti ya umeme imemsababishia hasara sio chini
ya milioni hamsini za kitanzania baada ya nyumba iliyokua
inatumika kama stoo ya vifaa vya production Benchmark
kuteketea yote kwa moto pamoja na vitu vilivyokuwemo ndani.
Madame amesema shoti ya umeme ilitokana na transfoma
ambayo ipo karibu na ofisi yao Kawe Dar es salaam ambapo
ofisi yote ilikua iungue ila shoti ilipofika kwenye ofisi kubwa
umeme ulijizima wenyewe kutokana na kifaa maalum
kinachoweza kuzuia shoti, hivyo nyumba ndogo ya stoo
iliyokua na vifaa vya productions vilivyokua vinatumika kwa
miaka kumi Benchmark production ndio ikateketea.
Tanesco wamethibitisha kweli kwamba ajali ya moto imetokana
na shoti ya umeme ambapo zimamoto walichelewa kufika
kwenye eneo la tukio kwa zaidi ya saa moja na nusu huku
wakisema foleni barabarani ndio iliyosababisha, hakukua
na njia ya kuuzima huo moto hivyo Madame Rita na timu
yake walibaki wakitazama tu nyumba ikiteketea.
Nilipomuuliza Madame kuhusu msg niliyotumiwa ya uwezekano
wa BSS kusimamishwa kutokana na hiyo ajali ya moto, namkariri akisema
“nahisi huyo jamaa labda alikua anataka hivyo lakini BSS haiwezi
kusimama kuruka hata siku moja, hata nikifariki”
picha na stori kwa hisani ya millardayo.com
No comments:
Post a Comment