Waziri wa dini wa Sudan Ghazi al-Sadiq Abdel Rahim ni
miongoni
mwa watu 31 waliouwawa katika ajali ya ndege.
Shirika la habari la Sudan limesema kuwa mawaziri wengine
wawili na pia
viongozi wa chama kinachotawala cha
Omar el-Bashir pia waliuwawa.
Ndege hiyo ya abiria ambayo pia ilikuwa imebeba wakuu
kadhaa wa kijeshi
ilianguka katika eneo la milima ya Nuba
Ndege hiyo ilikuwa ikielekea eneo la Kordofan ya Kusini
kwa sherehe za Eid
al-Fitr ili kuuaga mwezi mtukufu wa Ramadhan.
Mbali na waziri huyo wa maswala ya kidini
Ghazi al-Sadiq Abdel Rahim wengine
waliofariki katika
ajali hiyo ni mwenyekiti wa chama, Makki Ali Balayil,
waziri
wa vijana na michezo, na Issa Daifallah, waziri
wa utalii na wanayma pori.
Ndege hiyo ilianguka katika eneo la Talodi huko Kordofan
ya Kusini, ikiwa
imetoka mji mkuu Khartoum
Mji huo wa Talodi, uko kilomita 50 kutoka mpaka wa Sudan Kusini.
Taarifa za runinga ya taifa zinasema kuwa hali mbaya ya anga
iliizuia ndege
hiyo kutua na ilipojaribu mara ya pili iligonga mlima.
Afisa mmoja wa shughuli za ndege alisema kuwa ndege
hiyo ilikuwa ya aina ya
Antonov.
Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na ajali kadhaa mbaya za ndege.
Maafisa wa Sudan wamekuwa wakilalamika kuwa imekuwa
vigumu wao kupata vipuri
kwa sababu ya vikwazo vya Marekani.
No comments:
Post a Comment