Maafisa wa usalama wa Libya wamesema mabomu mawili
yaliyokuwa
kwenye gari yamelipuka katikati ya mji mkuu wa Tripoli,
moja karibu na ofisi ya wizara ya mambo ya Ndani na jingine
karibu na chuo
cha kijeshi.
Taarifa zinasema milipuko hiyo imeua watu wawili na kuacha
wengine wanne
kujeruhiwa katika chuo cha zamani
cha kijeshi cha wanawake.
Hili ni shambulio kubwa la kwanza kutokea tangu kuondolewa
madarakani kwa
aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo
Muammar Gaddafi mwaka jana.
Mkuu wa Usalama wa mji Tripoli amelaani mashambulizi
hayo yaliyolengwa kwa
watu wanaomuunga mkono rais wa
zamani wa nchi hiyo marehemu Mummar Gaddaf.
Katika hosptali ya Al Jalaa iliyopo Tripoli, Wesan Abu Alsoude
ambaye binamu
yake aliuawa amelaumu mamlaka kwa
kushindwa kuchuchukua hatua kuzuia shambulio
hilo.
No comments:
Post a Comment