Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ametangaza kipindi cha
maombolezo
nchini humo kufuatia mauaji ya wachimba madini thelathini na
wanne
yaliyofanywa na polisi,
wakati walipokuwa wakiandamana kudai malipo bora zaidi ya kazi.
wakati walipokuwa wakiandamana kudai malipo bora zaidi ya kazi.
Bwana Zuma pia ametaka tume ya uchunguzi ya kisheria ichunguze
mauaji hayo
katika mgodi wa madini meupe yaani PLATINUM
eneo la Marikana.
Wakati huohuo wachimba madini wameamriwa kurejea kazini
siku ya Jumatatu la
sivyo watafukuzwa kazi.
Lakini wengi wamesema kumaliza mgomo wao sasa ni sawa na
kuwadhalilisha
wenzao waliouawa.
Wanasema watarejea kugoma katika eneo la mgodi huo na wataendelea
kushinikiza
malipo bora zaidi ya kazi.
Hata hivyo chama cha wafanyakazi wa migodi cha NUM ambacho
kina uhusiano wa
karibu na chama tawala cha ANC - kinasema
wanachama wake wamekubali kurejea
kazini.
Mmoja wa wachimba madini hao Vuyisile Mchiza, amesema
atarejea kazini iwapo
idadi kubwa ya wenzake watakubaliana
kusitisha mgomo.
''Iwapo idadi kubwa watarejea kazini kesho, basi na mimi
nitakwenda''.
Anasema. ''Iwapo wengi hawatakwenda kazini
nami pia sitakwenda, kwasababu
sitaweza kufanya kazi wakati
wengine wakiwa bado wanaomboleza''.
No comments:
Post a Comment