Na Ibrahim Yamola na Irene Mossi, Mwananchi
(email the author)
Kwa ufupi
Kufuatia Rasimu ya Katiba, iliyopendekeza muundo wa Serikali tatu zitakazojitegemea.
Dar es Salaam. Jumuiya ya Umoja
wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM),imepinga mapendekezo ya Tume ya
Mabadiliko ya Katiba Mpya juu ya muundo wa Muungano kuwa wa Serikali
tatu.
Katibu Mkuu wa UVCCM, Martine Shigela,akizungumza
na waandishi wa habari jana alisema, kisheria muundo wa Serikali tatu
hauna tija hususani kwa Watanganyika.
Alisema kilichotakiwa kabla ya tume kupendekeza uwapo wake, ilitakiwa kutoa mapendekezo ya Katiba tatu ya kila upande.
“Kama kweli tume walitaka kutuonyesha tunataka
Muungano wa Serikali tatu, wangekuja na ‘Proposal’ mapendekezo ya Katiba
ya Serikali zote lakini si hivi wanavyofanya,”alisema Shigela na
kuongeza:
“Uwapo wa Serikali tatu ni kuongeza gharama za
uendeshaji na badala yake fedha hizo zinaweza kuelekezwa katika miradi
ya maendeleo yenye tija kwa taifa.”
Kauli hiyo ya UVCCM, inakwenda sambamba na ile ya
Chama hicho iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape
Nnauye kuwa chama hicho bado kinaamini kuwapo kwa muungano wenye muundo
wa Serikali mbili.
“Mapendekezo ambayo ndiyo msimamo wa chama
tulishayawasilisha kwenye Tume kuwa sisi tunapendekeza mfumo wa Serikali
mbili na siyo tatu wala moja,” alinukuliwa Nape alipokuwa akizungumza
na waandishi wa habari Dodoma mwezi uliopita.
Shigela alisema kisheria haiingii akilini kuundwa
kwa chombo cha Serikali tatu huku kukiwa na ukinzani juu ya katiba za
nchi washirika.
“Tutakuwa na Katiba ya Muungano,Zanzibar wanayo ya
kwao lakini Tanzania bara bado hawana Katiba hivyo kunatakiwa kila
upande uwe na katiba yake kabla ya kupata Katiba ya Muungano,” alisema
Shigela na kuongeza:
“Kupitia mawazo yatakayotolewa na vijana wetu kipi
wanakitaka kuhusu Muungano wetu tutakichukua na kukipeleka katika ngazi
ya juu kabla ya kukitolea ufafanuzi.”
Katibu Mkuu huyo alielezea kuwa umri wa kugombea
Ubunge kupandishwa kutoka miaka 21 hadi 25 ni kuwanyima fursa vijana
wengi kushika nafasi za uongozi.Alitolea mfano kuwa endapo mtoto ataanza darasa la kwanza akiwa na miaka
saba, atahitimu Chuo Kikuu akiwa na umri wa miaka 23 hivyo kuwa na
uwezo wa kushika nafasi ya kuongoza wananchi hivyo pendekezo hilo bado
halina tija kwani mtu akihitimu chuo anakuwa uwezo.
No comments:
Post a Comment