contact

husen

Saturday, May 26, 2012

KOCHA MPYA ENGLAND AANZA VYEMA



Roy Hodgson ameanza kuiongoza timu ya taifa ya England vyema
 kama meneja, kwa kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Norway,
 katika uwanja wa mjini Oslo wa Ullevaal.Bao la Ashley Young
 limempa nguvu meneja Hodgson katika mechi yake ya kwanza
 kama meneja wa EnglandKabla ya mechi hiyo, England ilikuwa
 imeshindwa kuishinda Norway katika kipindi cha miaka
 32 iliyopita.Ashley Young ndiye aliyefunga bao hilo la pekee
 katika mechi hiyo, katika dakika za mwanzomwanzo za mechi
 hiyo ya kirafiki. Hodgson alipata nafasi nzuri ya kuwatizama 
wachezaji wa England ambao ataweza kuwashirikisha zaidi
 katika juhudi zake za kuisuka vyema timu yake itakayoshiriki
 katika mashindano ya Ulaya ya Euro 2012, baada ya kuchukua
 kazi hiyo kutoka kwa Fabio Capello.Timu ya England
 ilionyesha nidhamu ya hali ya juu na anayoitazamia
 Hodgson, lakini wengi bila shaka wanafahamu timu
 ambayo England itakutana nayo, Ufaransa, tarehe 11
 mwezi Juni katika mji wa Donetsk, haitacheza sawa na
 timu waliyopambana nayo mjini Oslo.Lakini yalikuwa ni
 mazoezi ya kuridhisha kwa Hodgson, ambaye sasa ataweza
 kukinoa kikosi chake vyema zaidi katika mechi nyingine
 ya kirafiki katika uwanja wa nyumbani wa Wembley, 
Jumamosi ya tarehe 2 Juni, wakati England 
itakapoikaribisha timu ya taifa ya Ubelgiji.
Chanzo BBc Swahili

No comments:

Post a Comment