contact

husen

Sunday, May 20, 2012

TUZO ZA WANAMICHEZO 2012 KUHISANIWA NA SBL



Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano Kampuni ya SBL, Teddy Mapunda 
 akizungumza na Waandishi wa Habari,Serengeti Breweries (SBL), 
imetangaza rasmi kutoa udhamini wa kitita cha Sh. Milioni 150,
 katika tuzo za Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania
 (TASWA), hafla ambayo inatarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao.
Utoaji wa tuzo hizo utafanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee
 tarehe 14/06/2012 ambapo zaidi ya wageni 500 kuhudhuria.
  Akizungumza katika Mkutano huo Mapunda, amesema
 nia ya kudhamini tukio hilo kwa mara nyingine ni
 kuendelea kusaidia kuinua michezo nchini.
 Mapunda amesema kuwa kufanya hii ni sehemu mojawapo ya
 kuwatambua wanamichezo, lakini pia
 kupitia udhamini huo,
 wangependa kuwasaidia waandishi wa michezo kujaribu kuangalia
 ndani zaidi na kuleta mwanga na uelewa wa haraka kwa jamii
 juu ya michezo mbalimbali iliyopo hasa hapa kwetu Tanzania. 
 Udhamini huu utatumika katika maeneo mbalimbali kufanikisha
 sherehe hiyo kama vile chakula cha jioni, burudani,tuzo,
 vyeti, zawadi pamoja na mahitaji na matumizi mengine
 ili zoezi hili liwe nzuri na la kukumbukwa nchini Mkurugenzi
 huyo aliongeza kuwa kampuni ya bia ya Serengeti inajivunia 
kuwa mdhamini mkuu wa tuzo hizi kwa mwaka wa tatu sasa. 
SBL imekuwa mstari wa mbele katika kuchangia maendeleo
 hya michezo Tanzania na kwa sababu hiyo, inachukuliwa 
kama kampuni mfano wa kuigwa

No comments:

Post a Comment