contact

husen

Wednesday, June 20, 2012

KICHUPA CHA AY CHAFUNIKA MBELE MBELE


Siku chache baada ya kuachia video yake mpya ya ‘Party Zone’ msanii 
wa kimataifa wa nchini Tanzania, Ambwene Yesaya aka AY, vituo
 vikubwa vya runinga duniania vimeanza kuipiga video hiyo
 kwa fujo huku ikiipigia promo pia kwenye mitandao ya kijamii.
“Coming up on Crispy Fresh: Chris Brown, Coldplay ft Rihanna
, Kanye West, AY ft Marcochali ‘Party Zone’,Neyo, Usher &
 2freshLes,” iliandikwa jana kwenye ukurasa rasmi wa Twitter 
wa kituo cha Channel O cha Afrika kusini.
Kipindi hicho cha ‘Crispy Fresh’ hupiga video mpya zilizoifikia 
TV hiyo na katika lisi ya nyimbo hizi za jana kama zilivyotajwa kwenye
 orodha hiyo ni AY tu ndiye msanii kutoka Afrika ambaye wimbo wake
 upo katika awamu ya kipindi hicho na video zingine ni za wasanii wa Marekani.
Baada ya kuitambulisha video hiyo ambayo AY kamshirikisha 
Marco Chali, kituo hicho jana kiliandika tena, “Catch @AY ft Marcochali
 ‘Party Zone’ again at 17:43pm & 20:04pm on
 Channel O today, Original African.”
Wakati Channel O ikiendelea na promo hiyo ya video ya AY, 
kituo maarufu duniani kwa burudani cha nchini Ufaransa,
TRACE nacho kiliipa shavu video hiyo,
 “Comin up this hour— the brand new 
@Ay ft Marcochali – Party Zone! Stay tuned…”
Awali kabla ya jana TRACE Urban in Africa, iliitambulisha 
video hiyo kwa kuandika, “Stay tuned — coming up our
 EXCLUSIVE video – Ay ft marcochali “Party Zone” video!
 Only on TRACE Urban!”
Kwa promo hiyo ambayo ndo kwanza imeanza ni sahihi 
mtangazaji wa Clouds Fm Reuben Ndege kumuuliza hivi 
AY, “money still has a crush on you au tayari umeibebesha
 money mimba ya mapacha pair 4??? Na yeye kujibu.
 “Hahaha nishapiga mimba so big movement r gwan.”

source bongo 5

No comments:

Post a Comment