contact

husen

Wednesday, June 20, 2012

WASANII WA FILAMU WAPEWA CHANGAMOTO YA KUTOKA NA IDEA MPYA KATIKA KAZI ZAO


Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na Tasasi ya Gaba Arts 
mapema wiki hii wameendesha semina fupi kwa 
Wasanii wa filamu ili kuwajengea weledi katika
 eneo la uandishi bora wa miswada ya sinema
 (script writing).
Semina hiyo iliyoendeshwa kupitia programu 
ya Jukwaa la Sanaa kwenye Ukumbi wa BASATA 
ilijikita katika maeneo ya namna ya kuendeleza wazo 
hadi sinema ya kusisimua, namna ya kufikia 
hisia za watazamaji,ujenzi mzuri wa matukio,
kutengeneza wahusika na mfumo wa hadithi, Mwanzo,
 kati na hitimisho.

Akitoa mada kwenye programu hiyo maalum, Mkurugenzi 
wa asasi ya Gaba Arts James Gayo alisema kuwa, 
muda umefika sasa kwa wasanii wa filamu kusaka 
maarifa ili kutengeneza sinema zenye visa vipya, 
zenye weledi na zisizosukumwa na matakwa
 au maelekezo ya wasambazaji.
“Wenzetu kutoka nje wanatamani sana kupata 
vitu kutoka Afrika vyenye kuzungumza uhalisia 
wa maisha ya kwetu, wanataka kuona vitu vipya 
hivyo, katika uandishi wa muswada wa sinema suala 
la uhalisia na visa vyenye utofauti ni la msingi sana”
 alisisitiza Gayo.
Alizidi kueleza kuwa watazamaji wa sinema (filamu) 
huwa wana kawaida ya kuchoka pale wanapolishwa 
visa vya aina moja muda wote na akaonya kuwa
 kama wasanii hawatajikita katika kubuni visa vipya 
na vyenye kugusa uhalisia wa maisha yao wadau
 watasusia kununua.
“Ikiwa tutaendelea kutengeneza filamu zisizo na weledi,
 zenye visa vilevile na zenye kusukumwa na wasambazaji
 au haja ya kuchuma fedha za haraka tu watu 
watatuchoka na baadaye soko litakufa” alionya Gayo.

Gayo ambaye amepitia mafunzo ya utengenezaji
 filamu katika mataifa mbalimbali ikiwemo Marekani
 alitaja sifa za muswada (script) bora kuwa ni
 pamoja na kubeba wazo linalozalika kwenye jamii,
 visa vyenye uhalisia na vipya, utengenezaji mzuri wa
 wahusika na sifa zingine nyingi.
Kwa upande wake msanii wa mashairi Mrisho Mpoto
 ambaye alikuwa miongoni mwa waliohudhuria
 semina hiyo alisema kuwa, wasanii wa filamu 
wanahitaji kusaidiwa kwani kwa sasa soko la filamu 
limekuwa la kitumwa na lenye kuburuzwa na
 matakwa ya wasambazaji bila weledi.

Akihitimisha programu hiyo, Katibu Mtendaji wa
 BASATA Ghonche Materego alishauri wasanii wa
 filamu kujipanga kushirikiana na wasomi wenye weledi
 katika maeneo yao ili kuzalisha kazi zenye weledi la ubora.
E
“Tuna wataalam wengi katika Sanaa, wamebanana
 na mambo mengi lakini ni vema wasanii 
tukawatumia na kushirikiana nao katika kuboresha
 kazi zetu” alisisitiza Materego.

source dj choka

No comments:

Post a Comment