contact

husen

Thursday, June 28, 2012

OCTOPIZO RAPA ALIYETOA KONDOM "LETS DO IT"


Kuna wale ambao sasa hivi nchini Kenya 
wanamuona kama rapper bora kabisa kuliko wote.
 Kila ngoma anayotoa inamsogeza zaidi
 kwenye kulimiliki taji la king wa rap wa Kenya.
 Kijana huyu anatishia nafasi za wakali kama
 Collo na Abbas kwenye 
hip hop ya nchini humo.

Kwa sasa amekuwa gumzo nchini Kenya
 kwa kuzindua condom zake ziitwazo
 ‘let’s do it.
Kwa wale ambao wameshazitumia wanasema
 zimewapa mizuka ya ajabu. Kinachofurahisha 
ni kuwa condom hizi zinatoa 
mwanga ama zinawaka gizani.
 
Leo kupitia Twitter amesema condom hizo
 zitaingia sokoni hivi karibuni,
 "the first stock should be here in
 a months time what will take time
 is formalitiz and ish."

Anaamini kuwa katika dunia yale leo si rahisi 
kumwambia kijana aachane kabisa na ngono
 ili kuepuka virusi vya HIV hivyo ni afadhali
 kama wakitumia condom. Leo (June 28)
 ametweet, “in the 21st century telling
 a teenager or a 21yr old to abstsin ni ka
 kudial 555 and telling zack
 "we not brunging yu home"

 
Ni msanii wa hip hop kutoka Kibera, eneo
 maarufu sana jijini Nairobi wanapoishi watu wa
 hali ya chini kabisa, akina
 kajamba nani 
(the largest slum in Africa).

Ni mhasisi wa kundi la vijana liitwalo Y.G.B. 
(Young, Gifted, and Black), likiwa na rapper
 wenye vipaji, watunzi wa mashairi,
 wachoraji, wasanii wa graphics na dancers.

Alizaliwa mwaka 1987, kwa jina la 
HENRY OCHIENG. Amesoma shule ya msingi
 na sekondari hapo hapo Kibera pamoja na 
St. Mary's Changamwe College mjini Mombasa,
kabla ya kurejea Nairobi kujaribu
 bahati yake ya muziki.

Ni mtoto wa kwanza kwenye familia yao ya 
watoto wanne na pia ni baba wa mtoto
 mmoja wa kike aitwaye Tracy.

Akiwa na umri mdogo kabisa Octopizzo
 alifunzwa na maisha magumu ya Kibera lakini
 kuvutiwa kimuziki na wasanii kama Chino XL,
 Big L, KRS, Diabolic, EPMD, Copyright,
 CL Smooth, Immortal 
Technik, na Supernatural.
Ameshinda mashindano kibao ya freestyle
 nchini Kenya, 
kama G Pange Hip Hop Challenge
, Hip Hop Halisi Freestyle Challenge,
 na Usanii Kona Hip Hop Challenge.

 Octopizzo ameshapanda kwenye stage
 moja na wasanii wa kimataifa kama
 Dead Prezz (U.S.A.),
 Black Twang (U.K.), DJ Trouble Maker (U.S.A.),
 Bunt Face (U.S.A./Ethiopia),
 Malikah (Lebanon), Le Melanina (Colombia),
 Mad Maxamon (Germany),
 Restley Perez (Philippines), 
na Anne Khan (Germany). Na pia
 ameshaperform na wasanii wa Kenya
 wakiwemo Jua Cali, Nonini, P Unit,
 Wahu, Wyre, Jaguar, Jimmy Gait,
 Ukoo Flani, Point Blank,
 Mwafrika na Ness.
Mpaka sasa amesharekodu mixtape tatu, 
S.O.N. (Stragglers of Nairobi), Y.G.B.
 (Young Gifted and Black),
 na The White Shadow.
 Mwkaa 2008 S.O.N. ilikuwa mixtape iliyouza
 zaidi katika historia ya
 hip hop ya Kenya.

 Kwa uwezo wake, Octopizzo ana mustakali 
wa nguvu kwenye hip hop ya Kenya na
 Afrika Mashariki kwa ujumla. Anawaacha 
na fundisho vijana wanaopenda 
kufanya hip hop na kufanikiwa kama yeye,
 kuwa wanapaswa kufikiria zaidi ya kutoa
 ngoma na kupeleka radio.
 Wana uwezo
 wa kufikiria miradi ya kufanya na kuisaidia
 jamii wanayoishi kwa kujituma kuiletelea
 maendeleo na kuiweka kwenye
 ramani kwa kuitangaza kimuziki.


Source leotainment




No comments:

Post a Comment