contact

husen

Wednesday, June 27, 2012

PICHA YA MCHEZAJI WA UGANDA ALIYEFARIKI DUNIA

Mashabiki wa mpira wa miguu huko Sironko Uganda wamepata 

mshituko baada ya mchezaji kuzimia kwenye uwanja wa mpira

 na kufariki dunia wakati akipelekwa hospitali.

Simon Musika ana umri wa miaka 30 na alicheza kwenye hiyo 

mechi ya timu za mitaani kwa dakika 15 kabla ya kuzimia na 

kufariki dunia ambapo baada ya taarifa za kifo chake ilibidi

 mechi isimamishwe.

Ndugu wa marehemu walikusanyika kwenye uwanja wa mpira

 muda mfupi tu baada ya kifo cha mchezaji huyo.

 

source millardayo

No comments:

Post a Comment