contact

husen

Tuesday, August 21, 2012

MELES ZENAWI AFARIKI DUNIA

Alikuwa na umri wa miaka hamsini na saba na ni mmoja wa
viongozi wenye ushawishi mkubwa na ambaye utawala
wake ulikumbwa na utata barani afrika.
Hali yake ya afya imekuwa ikiangaziwa kwa majuma kadhaa
sasa ingawaje hakukuwa na thibitisho kuhusu alichokuwa akiugua hasa.
Taarifa ya baraza la mawaziri imesema kuwa Zenawi alikuwa
akipokea matibabu ng'ambo na afya yake ilikuwa ikiimarika
lakini akazidiwa siku ya Jumapili alipolazimika kurejeshwa
hospitali, ''Ingawaje madaktari wake walifanya kila wawezalo,
alifariki jana mwendo wa 23:40,'' taarifa hiyo imesema
Bwana Zenawi alikuwa kiongozi wa Ethiopia wakati taifa hilo
lilipoingia vitani na nchi jirani ya Eritrea mwaka 1998.
Meles Zenawi aliingia mamlakani mwaka 1991 baada ya
mapinduzi lakini akapokea sifa kutoka kwa mataifa ya magharibi.
Waziri mkuu wa Kenya raila Odinga ameiambia BBC kuwa
ana hofu kuhusu hali nchini Ethiopia kufuatia kifo cha Meles Zenawi.
Alisema kuwa hali nchini humo sio nzuri huku vita vya
kikabila vikiendelea kuwa tishio.
Bwana Odinga alimtaja Zenawi kama kiongozi mashuhuri
na mwenye elimu bora, aliyejitolea kuunganisha bara la afrika.
Naibu waziri mkuu Hailemariam Desalegn anatarajiwa
kuchukua mahala pake.

stori na picha kwa hisani ya bbc



                                .
                              

No comments:

Post a Comment