contact

husen

Tuesday, August 21, 2012

KIFO CHA ZENAWI AMANI KUENDELEA ETHIOPIA


Meles Zenawi
Serikali ya Ethiopia imesisitiza kuwa nchi hiyo ni tulivu licha ya kifo
 cha Waziri Mkuu wa nchi hiyo Meles Zenawi aliyekuwa
 na umri wa miaka 57.
Zenawi alifariki katika hosipitali katika mji mkuu wa Ubelgiji,
 Brussels, siku ya Jumatatu baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Mwili wake unasafirishwa kuelekea mako makuu ya Ethiopia
 Addis Ababa, na kipindi cha maombolezo ya kitaifa
 kimetangazwa nchini humo.
Vyombo vya serikali vimeripoti kuwa Makamu Waziri Mkuu
 Hailemariam Desalegn ndiye atakayeshika madaraka hadi
 wakati wa uchaguzi mwaka 2015.
Kifo cha Bwana Zenawi kimezua hofu ya kugombania
 madaraka ambayo ingeweza kuathiri amani ya nchi hiyo.
Ellen Johnson Sirleaf rais wa Liberia amemsifu Bwana Zenawi
 kuwa alikuwa kiongozi mahiri wa kurekebisha uchumi na
 pia kiongozi msomi na imara mwenye ushawishi mkubwa barani Afrika.
Naye waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga awali aliiambia
 BBC kuwa ana hofu kuhusu hali nchini Ethiopia kufuatia kifo
 cha Meles Zenawi kutokana na vita vya kikabila kuendelea kuwa tishio.
Licha ya kuwa kama mmoja wa viongozi wenye ushawishi
 mkubwa barani Afrika, lakini utawala wake ulikumbwa na utata barani humo.
Hali yake ya afya imekuwa ikiangaziwa kwa majuma kadhaa
kabla ya kifo chake ingawaje hakukuwa na thibitisho kuhusu
 alichokuwa akiugua hasa.
Taarifa ya baraza la mawaziri imesema kuwa Zenawi alikuwa
 akipokea matibabu ng'ambo na afya yake ilikuwa ikiimarika
 lakini akazidiwa siku ya Jumapili alipolazimika kurejeshwa
 hospitalini. Ingawaje madaktari wake walifanya kila wawezalo,
 alifariki siku ya Jumatatu usiku majira ya saa tano na nusu usiku.
Bwana Zenawi alikuwa kiongozi wa Ethiopia wakati taifa hilo
 lilipoingia vitani na nchi jirani ya Eritrea mwaka 1998.
Meles Zenawi aliingia mamlakani mwaka 1991 baada ya mapinduzi
 lakini akapokea sifa kutoka kwa mataifa ya magharibi.

picha na stori kwa hisani ya bbc

No comments:

Post a Comment