contact

husen

Sunday, August 19, 2012

MLIPUKO WA BOMU WAUWA WATU WAWILI NA KADHAA KUJERUHIWA

Athari ya mlipuko wa bomu mjini Tripoli

Maafisa wa usalama wa Libya wamesema mabomu mawili
yaliyokuwa kwenye gari yamelipuka katikati ya mji mkuu wa Tripoli,
moja karibu na ofisi ya wizara ya mambo ya Ndani na jingine
karibu na chuo cha kijeshi.
Taarifa zinasema milipuko hiyo imeua watu wawili na kuacha
wengine wanne kujeruhiwa katika chuo cha zamani
 cha kijeshi cha wanawake.
Hili ni shambulio kubwa la kwanza kutokea tangu kuondolewa
 madarakani kwa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo
Muammar Gaddafi mwaka jana.
Mkuu wa Usalama wa mji Tripoli amelaani mashambulizi
 hayo yaliyolengwa kwa watu wanaomuunga mkono rais wa
 zamani wa nchi hiyo marehemu Mummar Gaddaf.
Katika hosptali ya Al Jalaa iliyopo Tripoli, Wesan Abu Alsoude
 ambaye binamu yake aliuawa amelaumu mamlaka kwa
 kushindwa kuchuchukua hatua kuzuia shambulio hilo.

No comments:

Post a Comment